Na Asha Mwakyonde
MAMLAKA ya Bandari Tanzania TPA inatarajia kukamilisha mradi wa ujenzi
wa mtambo wa mafuta utakaorahisisha upakuaji wa mafuta bandarini ambao
umegharimu Tsh. bilioni 47.
Haya yamesema jijini Dar es Salaam jana na Waziri wa Uchukuzi na
Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe wakati wa ziara yake bandarini hapo
amesema alipofika TPA alikuta changamoto mbili kubwa.
Amezitaja changamoto hizo kuwa ni za fromita kutokupima kwa usahihi na
kutokuwapo kwa matenki ya serikali ya kuhifadhia mafuta hayo.
Waziri huyo amesema mitambo ya awali iliwasumbua ambapo Rais John Magufuli aliwaelekeza wanunue fromita mpya.
Mhandisi Kamwelwe ameeleza kuwa mweshoni mwa mwezi Oktaba mitambo hiyo
itakuwa imekamilika na kwamba watakuwa wameshasaini mitakatba ya ujenzi
wa matenki ya kuhifadhiwa mafuta.
Amesema kuna bidhaa kubwa za mafuta zinazopita badari za Dar es Salaam,
Tanga na Mtwara na kwamba awali walikuwa na mitambo ya kupitisha
mafuta kutoka kwenye meli kwenda kwenye matanki ambayo iliwasumbua.
“Nilipoteuliwa kuwa waziri wa uchukuzi nilikuwa naangalia mahesabu ya
lita ya mafuta iliyokuwa ikiuzwa kwa mwananchi wa kawaida bei ilikuwa
kubwa”,amesema Waziri Kamwelwe.
Waziri Kamwelwe amesema tayari tenda imeshatangazwa ya kujenga matenki
hayo meli haitakuwa ikikaa siku tano tofauti na awali ilivyokuwa ikikaa
na kulipa fidia ya dola 20,000.
Ameongeza kuwa kukamilika kwa matenki hayo mwananchi wa kwaida
atapunguziwa gharama tofauti na awali walikuwa akiuziwa bei ya juu ya
mafuta.
Alisema kuwa wanaendelea na ukaguzi wa mradi mkubwa wa ukarabati wa
upanuzi wa bandari ya Dar es Salaam kwa ujenzi magati nane ambayo moja
la magari na saba kwaajili ya makasha na mizigo ya nje.
Ameongeza kuwa wanapanua bandari ya Mtwara kwa kujenga gati moja kubwa
la mita 300 na wanatarajia kusaini mkataba kwa ajili ya kujenga magati
makubwa mawili katika bandari ya Tanga.
amesema pamoja na ukarabati wa bandari kuna miundombinu ambayo ni ya
lazima kurekebisha kutokana na maelekezo ya Rais Magufuli aliwaelekeza
wanunue skana za kutosha na tayari wamesha nunua.
Katika hatua nyingine Mhandisi Kamwelwe amezindua mifumo ya tehama ya
ERP na e-ofisi ambao utarahisisha ufanyaji wa malipo kwa njia ya
mtandao.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoka amesema Rais
Magufuli alifanya ziara Septemba 26 mwaka 2016 alitembelea eneo hilo
ambapo alizungumzia mambo mawili ya Fromita na skana.
Amesema kwa Dar es Salaam kuna mita 19, Mtwara 4 ambazo ni dizeli na
Petroli na kwamba Mtwara na Tanga ni kwa ajili ya dizeli na Petroli
lakini tuna mita mbili za pamoja ambazo ni kwa za mafuta ya ndege ya
taa.
Amesema kwa hapa Dar es Salaam kuna kila aina ya mafuta yanayokuja ndio
maana kuna mita 19 mafuta yanayopatika mbali na dizeli petroli, mafuta
ya ndege,taa na pia wataongeza mafuta ya kula, mazito, mafuta ghafi
,vilainishi na kutakuwa na mita kwa ajili ya gesi ya nishati.
“Faida zitakazopatikana ni pamoja na kuwa na upimaji wa uhakika zaidi,
kuondoa udanganyifu unaofanywana wafanyabiashara kwa kushirikiana na
wafanyakazi wachache kutoka taasisi za Umma”amesema.
Mhandisi Kakoko amesema mradi huo ulisainiwa Februari 28, mwaka jana na
baada ya mwezi mmoja Machi 29, alikabidhiwa mkandarasi kuanza kazi ya
kujenga mtambo huo.
Mkurugenzi huyo ameleza kuwa walikubaliana na Mkandarasi ifikapo
mwishoni mwa mwezi Septemba mradi huo uwe umekamilika na Oktoba utaanza
kufanyiwa majaribio na mafunzo kwa wafanyakazi watakao husika kutumia
mtambo huo.
Amesema gharama zilizotumika kumlipa mkandarasi katika mradi huo nidola
za kimarekani milioni 17.2 sawa na Tsh.bilioni 47 za kitanzania kwa mita
zote 29.
Mhandisi Kakoko amesema kuhusu uendeshaji wa mradi huo wamekubaliana na
taasisi 10 ambazo zitaleta wafanyakazi wao ili waweze kufanya kazi na
TPA na tayari wameanza mfumo wa pamoja wauendeshaji.
Amesema kuwa wameshirikiana na Ofisi ya Rais kwa pamoja wanashughulikia
eneo hilo kujenga na kwa uendeshiji wa mradi huo ambao utakuwa na
wafanyakazi 111.
'Mheshimiwa Waziri utakumbuka hayo ndo maelekezo ya serikali yanatokana
na hoja yako uliyoweka kwenye ngazi za juu za serikali kufanya
ushirikiano,'amesema.
Ameongeza kuwa wafanyakazi hao 111 kwa ajili vituo vitatu ambapo Tanga
17, Mtwara 17 na Dar es Salaam 77 wote watakuwa chini ya Mkurugenzi
Mkuu,Meneja kutoka TPA na watakuwa na maofisa mbalimbali kutoka katika
taasisi hizo 10.
No comments:
Post a Comment