HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 05, 2020

ANZISHENI CLUB ZA LISHE KUPUNGUZA UTAPIAMLO MASHULENI

 Na Lydia Lugakila, BUKOBA

Mkurungenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba mkoani Kagera ametoa muda wa wiki tatu kwa idara elimu msingi na sekondari katika halmashauri hiyo  kuhakikisha zinaunda club za lishe ili kupambana na tatizo la utapiamlo shuleni.


Agizo hilo limekuja kufuatia Mkurungenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba na Wwenyekiti wa kikao cha kamati ya lishe, Solomoni Kimilike kupokea taarifa iliyoeleza kuzingatiwa, club za lishe kuanzishwa katika shule ya msingi Maruku na Kemondo na kwa shule za sekondari mchakato kuendelea.


Kufuatia hali hiyo Mkurugenzi huyo amesema kuwa kufikia novemba 15 mwaka huu club za lishe kwa idara ya elimu msingi na sekondari zinatakiwa kukamilisha mchakato huo haraka iwezekanavyo.


Aidha afisa elimu sekondari wilaya ya Bukoba Nelson Sospeter ameahidi kutekeleza agizo hilo ikiwa ni pamoja na kushirikiana idara ya lishe kusaidia kuwapatia elimu


walimu pamoja na wanafunzi ili zianzishwe cluba za lishe mashuleni na kuleta tija katika elimu kwa upande wake kaimu afisa elimu msingi Bwana Joseph matope amesema kutokana na agizo hilo watajitahidi kutekeleza kwa wakati na kuwa hadi sasa tayari wamepiga hatua kubwa ikiwemo shule zote za msingi kuwa na vifaa vya kunawia mikono pamoja na kupata uji shuleni.


Mkurugenzi huyo amepongeza halmashauri hiyo kufanikisha pakubwa masuala ya lishe ikiwa ni pamoja na kununua mizani ya kisasa kwa ajili ya upimaji wa watoto.


Hata hivyo kwa upande wake Ufisa Lishe wilaya ya Bukoba Desdery Karugaba amesema kuwa halmshauri hiyo imekuwa ikifanya vizuri katika masuala ya lishe na kuwahimiza wazazi kufuata kanuni za afya kwa kunawa mikono wakati wa uandaaji wa chakula cha mtoto ikiwemo wazazi kuwabaini watoto wenye matatizo kwa kuepuka kutowaficha majumbani.

No comments:

Post a Comment

Pages