Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe.
Aboubakar Kunenge ameelekeza Maduka yote yanayouza Saruji kwenye Mkoa
huo kuhakikisha wanauza kwa bei elekezi isiyozidi Tsh 15,000 na
kumuelekeza Kamanda wa Polisi kanda maalumu ya Dar es salaam Lazaro
Mambosasa kuanza msako wa kuwakamata wote watakaokiuka agizo hilo.
RC
Kunenge ametoa agizo hilo wakati wa ziara kwenye viwanda vinavyozalisha
saruji na Maduka yanayouza saruji mkoani humo ambapo ameshangazwa kuona
uzalishaji wa saruji kwenye viwanda ukiendelea Kama kawaida na kuuza
kwa bei ya Tsh 12,500 lakini wauzaji wanauza kwa Bei ya Tsh 17,000
ambapo walipoulizwa kwanini wanauza kwa Bei hiyo wameeleza kuwa
wanauziwa kwa Bei ya Tsh 14,500 kutoka Mawakala jambo ambalo amelieleza
kuwa ni hujuma.
Kutokana
na hilo RC Kunenge ametoa maelekezo kwa Wizara ya Viwanda na biashara na
Afisa biashara wa Mkoa huo kupitia upya utaratibu wa uzalishaji na
uuzaji wa saruji kuanzia ngazi ya kiwandani Hadi kwa mtumiaji wa mwisho
ili kudhibiti upandaji holela wa bei.
Aidha
RC Kunenge amesema tayari ameandaa kikosi kazi kitakachopita kwenye
Maduka jijini humo na kuwakamata wote watakaouza saruji kwa Bei tofauti
na ile iliyoelekezwa.
"Katika
Mkoa huu chini ya Rais Dkt. John Magufuli hatuwezi kukubali upuuzi wa
aina hii, hatukubali hujuma hii na hatukubali uroho na ulafi wa watu
wachache wanaoumiza wananchi kwa maslahi yao binafsi, kuanzia wakati huu
saruji kwenye Mkoa huu isiuzwe zaidi ya Tsh 15,000" Alisema RC Kunenge
Kwa
upande wake Kamanda wa Polisi kanda maalumu ya Dar es salaam Lazaro
Mambosasa amesema jeshi hilo limejipanga ipasavyo kuhakikisha
wanafuatilia maeneo yote ya jiji hilo na kuwawajibisha wale wote
watakaokiuka maelekezo hayo.
No comments:
Post a Comment