Katibu Mkuu Wizara ya
Kilimo Gerald Kusaya ametoa wito kwa maafisa kilimo wa halmashauri za
mkoa wa Morogoro kuwafundisha wakulima kanuni bora za kilimo cha
umwagiliaji ili waongeze tija na uhakika wa kipato kufuatia serikali
kuboresha miundombinu.
Ametoa
wito huo leo wilayani Mvomero wakati alipokagua utekelezaji wa miradi
ya ujenzi wa ghala na skimu yaumwagiliaji ya kijiji cha Kagugu
inayotekelezwa na Mradi wa kuongeza thamani zao la mpunga (ERPP).
"
Wakulima lazima waoneshe kilimo bora kwa kutumia mbegu kidogo na maji
kidogo kufuatia mafunzo waliyopatiwa na wataalam wa kilimo cha
umwagiliaji ili tija ipatikanae na kuwasaidia kuongeza kipato kupitia
zao la mpunga" alisema Kusaya.
Katibu
Mkuu huyo ameagua mashamba ya mpunga kijiji cha Kagugu na kuwaelekeza
maafisa kilimo wa halmashauri kuwafundisha wakulima kilimo cha kisasa
ili mradi wa umwagiliaji uwasaidie kuongeza tija kwa kutumia eneo dogo
kisasa.
Kusaya
anafanya ziara ya kufuatilia utekelezaji wa mradi wa ERPP unatarajia
kukamilika mwishoni mwa mwezi huu Januari ili ukabidhiwe kwa wakulima
kupitia halmashauri baada ya Wizara yake kukamilisha miradi yote kumi na
moja.
Katibu
Mkuu huyo wa Kilimo aliongeza kusema Mradi wa Kuongeza tija na
uzalishaji wa zao la Mpunga (ERPP) unaotekelezwa kwa ubia na Benki ya
Dunia umefanikiwa kujenga maghala (5),skimu za umwagiliaji (5) na ujenzi
wa maabara moja ya kilimo kwa lengo la kusaidia wakulima kuongeza tija
katika zao la mpunga hatimaye nchi ijitosheleze kwa chakula na kipato
kwa wakulima.
"Lengo
la Rais wetu Dkt. John Pombe Magufuli ni kuona miradi hii ya kilimo cha
umwagiliaji inamnufaisha mkulima,hivyo tutapenda kuona mara baada ya
kuikabidhi kwa wakulima inakuwa endelevu" alisisitriza Kusaya.
Kusaya
aliongeza kusema wizara yake inaamini kuwa kilimo cha umwagiliaji ndio
mkombozi kwa mkulima kwani atakuwa na uhakika wa kuzalisha mazao yake
zaidi ya mara moja katika mwaka kutokana na uwepo wa mabonde yenye maji
na miundombinu ya kisasa.
Kwa
upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Albinius Mugonya alisema
wanaishukuru wwizara ya kilimo kwa kufanikisha kukamilisha miradi mitatu
ya ujenzi wa maghala mawili kijiji cha Mbogo Kwamtonga na Kagugu
pamoja na skimu ya umwagiliaji ya Kagugu ambazo zitakuza kiapato cha
wakulima.
"
Sisi wana Mvomero tuna miradi hii mitatu ambapo wakulima 5,673
watanufaika kwenye vijiji vya Mbogo Kwamtonga na Kagugu kwani tayari
tija imefikia wakulima wanazalisha tani 5 hadi sita za mpunga kwa hekta"
alisema Mugonya .
Mkuu
huyo wa wilaya alisema mkakati wa wilaya yake ni kuhamasisha ujenzi wa
viwanda vikubwa na vidogo ili kuongeza thamani ya zao la mpunga na
kuwafanya wakulima wauze mchele badala ya mpunga ili wapate kiapato
kikubwa.
Naye
mratibu wa mradi wa ERPP Mhandisi January Kayumbe alisema kwa sasa
miradiyote 11 katika wilaya za Mvomero, Kilosa na Ifakara ipo kwenye
hatua za ukamilishaji na kuwa ifikapo mwisho wa mwezi huu itakakuwa
tayari kukabidhiwa kwa wakulima.
Mradi wa ERPP ulianza kutekelezwa mwaka mwaka 2015 kwa gharama ya Dola za kimarekani milioni 22.91 toka Benki ya Dunia ukijusisha Tanzania Bara na Zanzibar.
Jumla ya miradi 11 ikiwemo ujenzi wa skimu 5 za umwagiliaji,ujenzi wa maghala 5 na ujenzi wa maabara moja ya mbegu inatekelezwa katika mkoa wa Morogoro chini ya ERPP.
No comments:
Post a Comment