HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 07, 2021

RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN ASHIRIKI KATIKA MAADHIMISHO YA SIKU YA KARUME DAY ZANZIBAR

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiweka Shada la Maua katika Kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar Hayati Abeid Amani Karume mara baada ya Dua iliyofanyika katika Ofisi Kuu za Chama cha Mapinduzi (CCM) Kisiwandui Zanzibar leo tarehe 07 April 2021 katika Siku ya Kumbukumbu ya (Karume Day).

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa na Rais wa Zanzibar Hussein Ali Mwinyi, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, pamoja na Viongozi wengine wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakiomba Dua mbele ya Kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar Hayati Abeid Amani Karume katika Ofisi Kuu za Chama cha Mapinduzi CCM Kisiwandui Zanzibar leo tarehe 07 April 2021 katika Siku ya Karume Day.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mara baada ya Dua Maalumu ya kumuombea Rais wa Kwanza wa Zanzibar Hayati Abeid Amani Karume katika siku ya Kumbukumbu ya Karume (Karume Day) iliyofanyika leo tarehe 07 April 2021 katika Ofisi Kuu za Chama cha Mapinduzi CCM Kisiwandui Zanzibar. PICHA NA IKULU.

No comments:

Post a Comment

Pages