NA HAMIDA RAMADHANI, DODOMA
MWENYEKITI
wa Vyama vya Siasa Tanzania John Shibuna amemuomba Rais wa Serikali ya
awamu ya sita Samia Suluhu Hassan akutane na vyama vya siasa ili waweze
kupata nasaha zake.
Shibuda
ameyasema hayo jana jijini hapa wakati akizungumza na waandishi wa
habari kuhusu tafakuri maalumu ya kuhitimisha kipindi cha maombolezo cha
aliyekuwa Rais wa Serikali ya awamu ya Tano Hayati Dk John Magufuli.
Amefafanua
kwamba hotuba ya kwanza ya Rais Samia ilionyesha na kuandikisha maono
na fikra sahihi za wadau wa tasnia ya siasa na imethibitisha mitazamo
ya kusimamiana kati ya serikali na wadau wa siasa.
“Kwa
kipindi kifupi ulichoongoza umeonyesha kuwa wewe ni kiongozi bora na
mbobezi kwa ujenzi na ufumbuzi kwa kuunda makutano kati ya fikra za
wadau wa vyama vingi na umaana wa hekima ya ujumbe wa hotuba yako ya
machi 19 mwaka huu,”amesema Shibuda.
Shibuda
amesema vyama vya siasa vinampongeza Rais Samia kwa kuwarejeshea
matumaini ya watanzania baada ya kumpoteza Hayati Dk Magufuli, kupitia
hotuba zake kumefanya kupatikana kwa matokeo chanya kwa ustawi na
maendeleo ya jamii,uchumi na taifa kwa ujumla na wananchi kurejesha
matumaini yao.
Aidha
ameipongeza serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan
kwa kuendeleza pale alipoishia Hayati Dk Magufuli huo ni uamsho mpya
unaokweza morali na kukuza hali mpya kwa umma kuwa rafiki na serikali ya
awamu ya sita.
Shibuda
amesema Hayati Rais Dk Magufuli ameacha dhana kwenye vichwa vya
watanzania vya kujitegemea kiuchumi na ndoto huru ya maendeleo na
ustawi wa jamii,uchumi na taifa.
Amesema
hayati DKt Magufuli ameondoka duniani akiwa amedhibiti dhana potofu na
ovu ya nchi kujengwa na wenye moyo na klul;iwa na wenye meno hususani
wenye mirija ya unyanyasaji wa mali na rasilimali za taifa kupitia watu
wa ndani na nje ya nchi.
“Hayati
Dk Magufuli amemaliza wajibu wake hapa duniani ameiacha serikali na
wananchi hivyo tuwe na misimamo thabiti ya kukataa vishawishi vya chui
waliovaa ngozi za kondoo wenye nia ovu na katili ya kudhuru na kudhurumu
maisha ya furaha na heshima za utu na uhai wa binadamu wa
Tanzania,”mesema Shibuda.
Mwenyekiti
huyo wa vyama vya saiasa ametoa usahuri kwa Waziri wa Fedha na Mipango
Mwigulu Nchemba kuibua uvumbuzi wa kisheria wa kusadikisha dhamila
njema ya serikali kulinda maslai ya kati ya benki na mteja anayeweka
pesa zake.
Amesema kodi
na VAT zinadhoofisha uchangamfu na ustawi wa biashara hivyo wizara ya
kilimo na wizara ya uwekezaji na wizara ya fedha kuwa na makutano mara
kwa mara kuunda sheria madhubuti zatakazo changia kukuza sekta muhimu
ya biashara hapa nchini ambayo itachangia kuongeza wigo wa ukusanyaji
kodi.
No comments:
Post a Comment