Alizindua maonyesho maalum tarehe 19 Juni 2021 Alliance Francaise jijini Dar es Salaam ikiwa ni maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani.
Maonesho hayo ya
yaliandaliwa na taasisi ya The Foundation for the Educational and
Environment Advancement of Tanzanians (FEET). Maonyesho hayo yalileta
hamasa kubwa na kdhihirisha ni kwa jinsi gani uharibifu wa mazingira
ulivyo ni hatari duniani. Hayo yote yaliambatana na maonyesho ya picha
kutoka kwa wanafunzi mbalimbali wa hapa nchini Tanzania, ikionyesha
jinsi uchafu wa plastiki ulivyo kwa maisha ya kila siku ya mwanadamu
pamoja na mazingira anayoishi.
Hayo yote yalifanyika kwa ufanisi
mkubwa na aliyekuwa nyuma ya maonyesho haya ni mwanafunzi wa mwaka wa
pili wa chuo cha University of Southern California (USC), Alyanz Nasser.
Alyanz
Nasser amekuwa na muamko na hamasa ya kutunza mazingira tangu akiwa na
umri wa miaka 15. Yeye pamoja na rafiki yake walizindua mfuko maalum
ambao ni rafiki kwa mazingira unaoitwa Envirobags.
FEET
ilianzisha kampeni wiki 12 zilizopita kwenye Instagram kwa lengo la
kupasa sauti kwa vijana wakati huu wa mabadiliko ya tabia nchi
ukiendelea. Zaidi ya shule 100 zilishiriki na wanafunzi walikuwa
wakichukua picha mnato pamoja na za video kwenye maeneo ya karibu nao
ambayo yanaonyesha uharibifu wa mazingira. Nia ya kampeni hii ilikuwa ni
kutoa hamasa na kuonyesha ni kwa jinsi ngani binadamu wanaharifu
mazingira na jinsi wanafunzi wanaweza kushiriki kubadilisha hali hiyo.
FEET
pia itapanda miti 20,000 aina ya Jacaranda hapa Tanzania. Juhudi hizi
zitasaidia jamii ya Tanzania kwa kusaidia kuongeza hali nzuri ya
mazingira, upungufu wa chakula pamoja na kuongeza kipato. Njaa, ukataji
holela wa miti, upungufu wa chakula, ushindani wa mali asili, njaa na
uhamiaji halole na haramu zimechangia sana uharibifu wa mazingira. Miti
ni mali asili ambayo itatatua changamoto zote hizo.
FEET pia ina
mpango wa kupanda asilia ambayo usaidia kuimarisha ardhi na kuifanya iwe
na faida Zaidi na imara na hivyo kuongeza bioanuwai, wakati mbinu
salama za kilimo zikihimiza kilimo endelevu pamoja na utafutaji wa
maisha.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Liberata Mulamula, Waziri wa Nchi Ofisi ya Raisi Ummy Mwalimu, Balozi
wa Ufaransa hapa nchini Frederic Clavier, Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi
ya Makamu wa Raisi Dkt Andrew Komba pamoja na mabalozi watatu wa
mazingira walikuwepo.
Waziri Liberata Mulamula alisema, ‘Utunzaji
wa mazingira, uwe mdogo au mkubwa ukindwa kwa pamoja utasaidia
kubadilisha maisha ya binadamu wanaotengemea mazingira. Nakushukuru kwa
vile unavyofanya na vile imesaidia nchi kwenye kukabiliana na mabadiliko
ya tabia nchi. Umechangua njia sahihi. Nawapongeza FEET pamoja na
washirika wake.’
Waziri Ummy Mwalimu alisema, ‘Tunayo taarifa
kwamba FEET itapanda miti 20,000, tutafanya kazi pamoja nanyi kama
serikali za mtaa kuhakikisha kuwa lengo lenu linafanikiwa’.
Balozi
Frederic Clavier pia alitoa pongezi kwa FEET, ‘Sisi kwa pamoja
tunatakiwa kufanya kazi kulinda mazingira yetu kutokana na mabadiliko ya
tabia nchi, ukataji ovyo wa miti pamoja na uchafuzi wa mazingira’.
Mkurugenzi
wa Mazingira Dkt Andrew Komba alisema kuwa anatambua juhudi za kila mtu
za kulinda mazingira pamoja na kupambana na uchafuzi wa mazingira.
Honorable Minister Liberata Mulamula delivering a speech at FEET's Ecosystem Restoration Campaign Launch.
Alyanz Nasser - FEET founder delivering a speech at the Ecosystem Restoration Campaign
From
Left to Right:His Excellency Frederic Clavier, Honorable Minister Ummy
Mwalimu, Alyanz Nasser - FEET Founder, Mariam Ditopile Environment
Ambassador, at the FEET event.
Alyanz explaining the purpose of the exhibition to the VIP guests.
Alyanz with his tutor Moses in the Exhibition Hall
School Students who were the winners of FEET's ecosystem restoration campaign
No comments:
Post a Comment