Na Asha Mwakyonde, Da es Salaam
WANAFUNZI wanaosoma umeme wametakiwa kujitokeza kwenye viwanya vya kimataifa vya mwalimu nyerere vilivyopo barabara ya Kilwa ambapo maonyesho ya kimataifa ya 45 ya sabasaba yanafanyika na kutembelea kwenye banda la chuo cha uwalimu cha mafunzo ya ufundi stadi MVTTC EETAMOROGORO) ili kupata elimu kuhusu umeme.
Akizungumza na waandishi wa habari jana kwenye viwanja hivyo vya maonyesho wilayani temeke Frank Urio ambaye ni mhandis kutoka chuo hicho kilichopo mkoani Morogoro alisema kuwa wapo katika maonyesho hayo na wamekuja na kifaa kipya kuhusu umeme.
Amesema kuwa kuna changamoto kubwa sana kwa wanafunzi ambao wanakwenda kufanya mafunzo kwa vitendo na ndio maana kupitia maonyesho hayo wamekuja na kifaa ili kuweza kuwapa elimu stahiki na kifaa hicho ni teknolojia mpya na ndani yake kuna mafunzo ya aina mbili ambayo ni electronic mashine nanyingine.
“Ndugu waandishi kikubwa kupitia maonyesho haya tunawaomba wanafunzi waje ,na wajitokeze kwa wingi ili waje kupata elimu stahiki kuhusu umeme na kama mnvyojua changamoto za umeme kwahiyo tupo hapa hadi julai 13 hivyo wajitokeze.”amesema mhandisi Urio
Ametoa wito kwa wanafuzni ambao wamesoma umeme waje ili wafundishwe kujua namna ya kuona vifaa hivyo jinsi vinavyo kufanya kazi ili akiwa katika maeneo yake yakazi asikutane na changamoto kubwa.
Naye Sophia Tuka ambaye ni mkufunzi mwandamizi chuoni hapo akizungumzia kozi ambazo zinatolewa chuoni hapo hususani mwaka huu wa masomo alisema kuwa chuo hicho kinatoa kozi mbalimbali za ualimu na wanaandaa walimu wanaofundisha ufundi.
Amesema katika chuo chao wanatoa elimu ya ufundi katika ngazi ya cheti na pia wanatoa mafuzo kwa ngazi ya astashahada (Diploma) na mwezi wa tisa masomo yanaaza hivyo wanafunzi wajitokeze na kujiunga ili kuweza kupata elimu ya ufundi
July 10, 2021
Home
Unlabelled
Wanaosomea umeme watakiwa kutembelea banda la chuo cha uwalimu MVTTC
Wanaosomea umeme watakiwa kutembelea banda la chuo cha uwalimu MVTTC
Share This
About HABARI MSETO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.


No comments:
Post a Comment