HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 30, 2021

AFISA MTENDAJI MKUU NFRA AWEKA WAZI UTEKELEZAJI MRADI WA KUONGEZA UWEZO WA UHIFADHI NAFAKA KATIKA MAENEO NANE

Saymon Kobilesky Mhandisi Mjenzi wa Maghala ya Kuhifadhia Chakula mjini Sumbawanga kutoka Kampuni ya Unia Araj Poland akitoa Maelezo kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Bw. Bw. Milton Lupa wakati alipotembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa maghala ya kuhifadhia chakula mjini Mpanda mkoani Katavi  hivi karibuni. Kushoto ni Marwa Range Kaimu Meneja wa NFRA Kanda ya Sumbawanga.

Proches Kiwango Fundi Sanifu wa Mradi wa Maghala ya NFRA Mpanda akitoa maelezo kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Bw. Milton Lupa wa pili kutoka kushoto wakati alipokagua mradi huo unaotekelezwa na Kampuni ya Unia Araj Poland hivi karibuni, kushoto ni Marwa Range Kaimu Meneja wa NFRA Kanda ya Sumbawanga na Katikati ni Bw. Hudson Kamoga Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Kilimo

Muonekano wa mradi wa ujenzi wa maghala ya kuhifadhia chakula Mpanda mkoani Katavi.

Proches Kiwango Fundi Sanifu wa Mradi wa Maghala ya NFRA Mpanda akitoa maelezo kwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Bw. Bw. Milton Lupa wa wakati alipokagua mradi huo unaotekelezwa na Kampuni ya Unia Araj Poland mjini Mpanda mkoani Katavi hivi karibuni.

Agustino Mwadasi Mhandisi Mkazi wa Mradi wa ujenzi wa Maghala ya kuhifadhia ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Vwawa Mbozi mkoani Songwe kutoka TBA akitoa maelezo kwa Bw. Hudson Kamoga Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Kilimo wakati alipotembelea mradi huo na kuona hatua mbalimbali za utekelezaji hivi karibuni kushoto ni Eva Michael Kwavava Kaimu Meneja wa NFRA Songwe.

Proches Kiwango Fundi Sanifu wa Mradi wa Maghala ya NFRA Mpanda akitoa maelezo kwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Bw. Bw. Milton Lupa katikati wakati alipokagua mradi wa Maghala ya NFRA unaotekelezwa na Kampuni ya Unia Araj Poland mjini Mpanda mkoani Katavi hivi karibuni. kushoto ni Hudson Kamoga Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Kilimo.

 

...............................................

Na Mwandishi wetu, Mpanda Katavi

 

AFISA Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Milton Lupaa amesema Wakala huo unatekeleza mradi wa ujenzi wa maghala ili kuongeza uwezo wa hifadhi nafaka katika maeneo nane hapa nchini.

 

Akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea ujenzi wa miradi hiyo iliyopo mjini Mpanda, Sumbawanga, Songwe, Makambaku, Babati, Dodoma na kujionea shughuli zinazoendelea katika ujenzi wa maghala hayo makubwa, yenye uwezo wa kuongeza uwezo wa kuhifadhi zaidi ya tani 250,000. Bwana Lupa amesema, lengo ni kuongeza uwezo wa Taasisi na kupunguza adha ya wakulima kubaki na mazao yao nyumbani kwa kukosa soko au mahali pa kuhifadhi mara baada ya kuvuna.

 

"Gharama za mradi huo ni dola za Marekani milioni 67 ambazo kati yake dola milioni 55 ni mkopo wa masharti nafuu kutoka serikali ya Poland na dola milioni 12 ni fedha za ndani kutoka serikali. Ujenzi unatekelezwa na wakandarasi wawili wote kutoka nchini Poland ambao ni kampuni ya M/S FEERUM S.A ambayo inatekeleza maeneo matano na kampuni ya Unia Sp.zo.o ambayo inatekeleza maeneo matatu. Huku mhandisi mshauru wa mradi ni Wakala wa Ujenzi wa Tanzania(TBA).

 

"Katika maeneo ambayo wakandarasi hao wanatekeleza mradi zipo faida kwa watanzania kama vile wananchi kupata ajira ambapo wakandarasi wazawa wanaajiriwa kama "Sub Contracors" na shughuli zingine za kiuchumi zinaendelea wakiwemo Mama lishe, Baba Lishe na baadhi ya vibarua ambao wanafanya kazi za kusaidia mafundi pamoja na wataalam wetu kujiongezea ujuzi zaidi katika fani zao za uhandisi,"amesema.

 

Ameongeza kuwa, mradi huo ukikamilika utaongeza tani laki 250,000 za uhifadhi wa chakula na kufikisha tani laki 501,000 ambapo kwa sasa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) ina uwezo wa kuhifadhi tani 251,000.

 

Pia, uwekezaji huo wa maghala una tija kubwa kwa serikali, wakulima na wananchi kwa sababu ni jukumu la NFRA kununua chakula kwa wakulima na kukihifadhi ili kunapotokea changamoto ya njaa au bei ya mazao kwa wakulima kuwa chini NFRA iyanunuwe na kuhifadhi.

 

"Kwasababu hawa wakulima wa chini hawana uwezo wa kuhifadhi mazao hayo kitaalam hili linafanyika kwa sababu ya kuwalinda wasitetereke kiuchumi katika shughuli nzima ya kilimo chao. Kuhusu ununuzi wa mahindi, Bwana Lupa amesema NFRA inaendelea kununua mahindi kwa wakulima katika vituo vyake vyote hapa nchini na tayari imenunua zaidi ya tani elfu 40,000 na inanunua mahindi kwa vyama vya ushirika na mtu moja mmoja. 

 

 "Utaratibu wa kununua umeshawekwa ambapo kila mkulima atauza mahindi kati ya gunia 1 mpaka magunia 300. Serikali inawalenga zaidi wakulima wa kawaida kwa sababu uwezo wao wa kuhifadhi mahindi ni mdogo hivyo ni muhimu kuwalinda ili waweze kuendelea na kilimo chao katika msimu ujao,"amesema.

 

Amesema, vifaa vyote vinavyohusika katika ununuzi wa mazao hayo vimeshapelekwa katika vituo vyote vya kununulia na kama kutakuwa na changamoto yoyote wakulima wasisite kutoa taarifa zishughulikiwe mara moja ili kutokwamisha zoezi la ununuzi wa mazao hayo.

 

Amewaomba, wakulima hao kuwa watulivu na kufuata maelekezo na taratibu watakazopewa na maofisa wa NFRA ili waweze kuuza mahindi yao yote kwa utaratibu uliowekwa ambapo pia amewataka kutokuwa na wasiwasi wowote katika zoezi zima la ununuzi wa mahindi yao.

No comments:

Post a Comment

Pages