HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 30, 2021

AZAKI ZATAKIWA KUHAMASISHA SENSA YA WATU NA MAKAZI

 Jasmine Shamwep, DODOMA

KAMISAA wa Sensa Tanzania Bara ambaye pia ni Spika wa Bunge Mstaafu Anne Makinda amezitaka Asasi za kiraia nchini (AZAKI) kutoa Elimu kwa Jamii kuhamasisha kikamilifu katika zoezi la Sensa ya watu na makazi linalotarajiwa kufanyika Agosti 2022.

Anne Makinda ameyasema hayo leo wakati akitoa mada ya uelimishaji na uhamasishaji wa masuala ya sensa kwa Asasi za Kiraia Katika Mkutano wa wiki ya AZAKI unaoendelea Jijini hapa ambapo ameeleza umuhimu wa sensa na wajibu kwa kila mtanzania kuisadia Serikali kupata taarifa za msingi zitakazosaidia mchakato wa utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya mwaka 2025, mageuzi ya masuala ya afya na jamii, pamoja na ufuatiliaji wa ajenda za maendeleo za kimataifa.


"Ninyi mnaaminika Sana na wananchi hivyo tunaomba muisaidie Serikali katika kuieleimisha Jamii kuhusiana na umuhimu wa sensa kwani baadhi ya watu bado Wana Mila Potofu kuhusiana na sensa hivyo kwakufanya hivyo isaidia wananchi kuwa na uelewa.",Alisema

"Sensa ni muhimu na inafanyika kila baada ya miaka kumi,nyinyi watu wa AZAKI ni wadau namba moja na mnaaminika na wananchi na mnakutana nao Kila siku ,tunatakiwa kutoka kwenye uchumi wa kati tuendende zàidi tufanane na wenzetu,"alieleza.

Aidha amesema Sensa ya Watu na Makazi ni zoezi la kitaifa linalofanyika kila baada ya miaka 10 ambapo Sensa ya mwisho kufanyika nchini ni ile ya mwaka 2012 hivyo Sensa ya mwaka huu itakuwa ni sensa ya sita kufanyika nchini baada ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964. Sensa nyingine zilifanyika mwaka 1967, 1978, 1988, 2002 na 2012.

"Sensa ya watu na makazi ni utaratibu wa kukusanya, kuchambua, kutathimini na kuchapisha na kusambaza takwimu za kidemographia, kiuchumi na kijamii kuhusiana na watu wote na makazi yao katika nchi kwa kipindi maalum,kwa maana nyingine, sensa ni zoezi maalum lenye lengo la kupata idadi ya watu wote katika nchi,


Katika hatua nyingine Kamisaa huyo wa sensa amesema Sensa hiyo itazingatia taarifa za idadi ya watu katika kusaidia kupanga maendeleo ya nchi ambayo huakisi matakwa ya watu katika ngazi husika na kusaidia kwenye uwiano wa mgawanyo wa rasilimalimali.

"Taarifa za sensa zitawezesha serikali kujua ongezeko la idadi ya watu, kwa mgawanyo na viashiria vingine, ambavyo ni muhimu kwa usimamizi wa mazingira,msingi wa utawala bora na ujumuishaji wa demokrasia,takwimu hizi zinahitajika kwa ajili ya ugawaji wa majimbo ya uchaguzi kwa ufanisi, kurekebisha mipaka ya kiutawala katika serikali za mitaa,"alifafanua.

Kwa upande wake Mtakwimu Mwandamizi,Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) David Mwaipopo
alitumia nafasi hiyo kuwaeleza Wana AZAKI kuwa sensa ya mwaka 2022 kama zilivyo sensa zilizopita itatumia aina mbili kuu za madodoso ambazo ni dodoso refu litakalotumika kuhoji asilimia 30 ya maeneo yote ya kuhesabia watu na Dodoso fupi litakalotumika kuhoji kwenye asilimia 70 ya maeneo yote ya kuhesabia watu.

Aliyataja madodoso mengine kuwa ni la Taasisi ambalo ni mahsusi kwa ajili ya wasafiri, waltakaolala mahotelini na nyumba za wageni, na waliolazwa hospitalini na dodoso la Wasio na Makazi maalum ambalo ni mahsusi kwa watu wote wanaolala maeneo yasiyo rasmi, kwenye baraza za majengo mbalimbali, kwenye madaraja na maeneo mengine.


"Tunaomba AZAKI mshiriki kikamilifu kuelimisha jamii tufikie malengo,sisi kama Ofisi ya Takwimu tumejipanga vizuri kwa kutumia rasilimali chache zilizopo ili kukamilisha kwa wakati shughuli zote za maandalizi ikiwamo kazi ya utengaji wa maeneo ya kuhesabia watu katika ngazi ya kitongoji na mtaa ambayo ndiyo msingi wa kufanikisha sensa kwa ubora,"alieleza.


Aidha zoezi la Sensa ambalo litqfanyika Mwakani litahusisha anuani za Makazi  ambayo itasaidia kufahamu mtu alipo  lengo likiwa ni kufanikisha zoezi hilo.

No comments:

Post a Comment

Pages