HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 06, 2021

Bidhaa za ngozi zinazozalishwa nchini zina ubora-Woiso


Baadhi ya bidhaa zinazozalishwa na Kiwanda cha Woiso Original Product.

Baadhi ya bidhaa zinazozalishwa na Kiwanda cha Woiso Original Product.


 

PATRICIA KIMELEMETA

MKURUGENZI Mtendaji wa Kiwanda cha Woiso Original Product, Kenneth Woiso amewashauri watanzania kununua bidhaa zinazozalishwa nchini kwa sababu zina ubora kulikobidhaa zinazotoka nje ya nchi na kuuzwa kwa gharama nafuu.

Akizungumza hivi karibuni, Woiso alisema kuwa, viatu vinavyotengenezwa nchini vinatumia ngozi origino  ambayo inazalishwa hapa nchini, lakini viatu vinavyoyoka nje ya nchi, baadhi yao vinatumia ngozi ghushi iliyochangwa na plastiki.

Alisema kuwa, kutokana na hali hiyo, watanzania wanapaswa kupewa elimu ili waweze kutofautisha kati ya ngozi ghushi na ngozi origano hata wanapoenda dukani wanachagua kitu bora ambacho kimetengenezwa kwa ngozi origino.

"Watanzania wengi wanapebda kununua bidhaa zilizotengenezwa nje ya nchi wakiamini kuwa ni bora zaidi kuliko bidhaa zinazotrngenezwa ndani ya nchi, wakati sio kweli, bidhaa zetu ni bora na zinatrngrnezwa kwa kiwango cha juu kwa kutumia ngozi origino na sio ngozi ghushi," alisema Woiso.

Aliongeza kuwa, ndomana bidhaa za nje ya nchi zinauzwa bei nafuu ili kuvutia wateja kwa sababu haziwezi kudumu muda mrefu kutokana na ubora wa kiwango cha chini.

Alisema kuwa, hivyo basi wakati umefika wa Serikali kushirikiana na wadau mbalimbali ili kutoa elimu kwa wananchi waweze kutambua ubora wa bidhaa za ngozi zinazozalishwa nchi na kutofautisha na bidhaa za ngozi zinazotoka nje ya nchi

Alisema kuwa, viatu anavyotengeneza ananunua ngozi kutoka kwenye viwanda vya ndani ya nchi vinavyotengrneza bidhaa hizo, jambo ambalo limesaidia kuwa na viatu bora vinavyodumu muda mrefu kuliko vile vya nje.

"Nanunua ngozi kutoka kwenye viwabda vya hapa nchini ambavyo na vyenyewe vinanunua ngozi kutoka kwa wafugaji na kupeleka kiwandani kwa ajili ya kuiboresha na kutuuzia,ndomana viatu vyetu vinakaa muda mrefu kutoka viatu vinavyotoka nje ya nchi zenye majina makubwa," alisema.

Alisema mpaka sasa, bidhaa zinazozalishwa kwenye Kiwanda hicho zinauzwa katika nchi mbalimbali zikiwamo za Afrika Mashariki na Dubai, hali ambayo imesaidia kukuza soko la nje na kuitangaza nchi kibiashara.

Alisema kuwa, mkakati uliopo ni kuendelea kutoka elimu kwa wananchi Iwaweze kutofautisha kati ya ngozi bora na ngozi ghushi, jambo ambalo litasaidia kuongeza mauzo kwenye soko la ndani na serikali kupata mapato.

"Kuna baadhi ya nchi maarufu wanatengeneza bidhaa za ngozi ghushi na kuzileta nchi, tena zinauzwa kwa bei nafuu na wateja wanakimbilia, lakini hazidumu muda mrefu kwa sababu zimetengenezwa chini ya kiwango," alisema.

Kiwanda cha Woiso kunazalisha bidhaa mbalimbali zikiwamo viatu, mapazia, samani za ndani na magodoro.

No comments:

Post a Comment

Pages