HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 12, 2021

KAMPUNI YA TEMBO NICKEL KUTOA AJIRA 1000

   

Meneja Mkazi wa Kampuni ya Tembo Nickel hapa nchini Benedict Busunzu akizungumza wakati wa utambulishaji wa Mradi huo.

 

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Charles Mbuge akitoa hotuba katika hafla fupi ya kuwapokea wawekezaji.


 

Na Lydia Lugakila, Bukoba

 
Kampuni ya Tembo Nickel yatarajia kufanikisha kuzalisha madini ya Nickel ndani ya miezi 38 kwa mara ya kwanza hapa nchini katika wilaya ya Ngara mkoani Kagera  huku ajira  900 hadi 1000 zikitarajiwa kutolewa baada ya hatua ya uzalishaji.

Kauli hiyo imetolewa na Meneja mkazi kutoka kampuni ya  Tembo Nickel hapa nchini  Benedict Busunzu katika hafla fupi ya kujitambulisha rasmi kwa Mkuu wa  Mkoa wa Kagera Charles Mbuge iliyofanyika katika ukumbi wa Mkoa huo.

Busunzu amesema kuwa uwepo wa Nickel jamii Mkoani Kagera hasa wananchi waishio wilayani Ngara  itawanufaisha kutokana na shughuli zitakazofanyika ambapo ndani ya zaidi ya miaka 3 wanatarajia kutumia zaidi ya shilingi tilioni 3 kwa ajili ya ujenzi na uanzishaji wa shughuli mbali mbali ikiwemo kujenga mgodi wilayani Ngara  na wilayani Kahama Mkoani Shinyanga.

Amesema kuwa kwa Sasa kazi kubwa iliyobaki ni kuzungumza na wananchi wa wanaoishi karibu na eneo hilo ili kuona namna ya kuanza utaratibu wa uthamini kusha kuwahamisha wananchi hao ili kuruhusu shughuli hiyo kuanza Mara moja baada ya kukamilisha vigezo muhimu.

Aidha amezitaja shughuli wanazotegemea kuanza nazo kuwa ni kucholonga mwamba ili kufanya tafiti wa baadhi ya mashapu ambayo yatatumika katika ujenzi wa mgodi Kahama huku akieleza kuwa kampuni haitakuwa peke yake katika uchimbaji na kuzalisha makinikia ya Nickel ambayo hayataenda nje kutokana na kujenga mtambo wa uchenjuaji ili.

Kwa upande wake mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Charles Mbuge ametaja kufurahishwa na suala hilo la uwekezaji na kwa kampuni ya Tembo Nickel ambayo ilipewa kibali cha kuchimba madini mnamo oktoba 27 mwaka na kuongeza kuwa  ni miaka 40 sasa tangu uanze kufanyika utafiti huku akiwahimiza wananchi wilayani Ngara kuchangamkia fulsa hiyo, kuahidi kuwasimmia ili wapate haki yao na kuwatadhalisha wajanja watakaojaribu kuweka vikwazo katika mradi huo kula nao sahani moja.

Ikumbukwe kuwa kampuni ya Tembo Nickel imeundwa kwa kushirikiana baina ya kampuni ya Kabanga Nickel Co-operation iliyoko uingereza pamoja na serikali ya Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Pages