HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 12, 2021

Koka achangia kiasi cha shilingi mlioni 2 kwa shule nne za msingi msangani

  Mbunge wa jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka akizungumza na wananchi  wakati wa ziara yake ya kikazi kwa lengo la kubaini chanagmoto zilizopo pamoja na kukagua miradi mbali mbali ya maendeleo.

 

 

VICTOR MASANGU, KIBAHA 

 

KATIKA kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya sita Mama Samia Suluhu Hassan Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry koka ameamua kuchochea maendelea katika sekta ya elimu kwa kuchangia kiasi cha shilingi milioni  mbili  kwa  shule  nne za msingi  zilizopo kata ya Msangani  kwa lengo la kuboresha miundombinu ya madarasa ili wanafunzi waweze kusoma katika mazingira rafiki na kuondokana na adha ya kusoma kwa mlundikano.

Koka amechangia fedha hizo wakati wa mkutano wake wa hadhara na wananchi kutoka mitaa mbali mabli iliyopo katika kata ya Msangani   ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kikazi yanye lengo la kuweza kuzungumza na wakazi na kusikiliza changamoto mbali mbali zinazowakabili pamoja na kukagua miradi mbali mbali ya kimaendeleo katika sekta ya elimu, miundombinu ya barabara na mambo mengine ya kijamii.

 

Koka alisema kwamba lengo lake kubwa ni kuhakikisha anaweka mipango madhubuti amabyo itaweza kusaidia kuboreresha sekta ya elimu hasa katika shule ambazo zipo pembezoni mwa mji wa Kibaha na kwamba atashirikiana na  serikali pamoja na wadau mbali mbali wa elimu ili kuleta mabadiliko chanya katika sekta ya elimu ikiwemo miundombinu ya majengo ya madarasa, nyumba za walimu sambamba na huduma ya upatikanaji wa matundu ya vyoo.

 

“Kitu kikubwa napenda kuchukua fura hii kuwashukuru wananchi ambao kwa namna moja au nyingine ambao mliweza kunichagua tena kwa mara nyingine nah ii inaonyesha kwamba tupo pamoja katika suala zima la kuhakikisha tunakuwa pamoja na kushirikiana bega kwa bega katika kuwaletea chachu ya maendeleoa katika Nyanja mabali mbali hasa katika suala  la elimu na ndio maana nimeamua kuchangia kiais cha shilingi milioni mbili kwa kwa shule nne za msingi zilizopo katika kata ya Msangani,”alisema Koka.

Aidha aliongeza kuwa fedha hizo ambazo amezitoa katika shule nne za msingi ni pamoja na shule ya msingi Kidenge A pamoja na kidenge B sambamba na shule ya Msangani pamoja na madina ambapo kila shule amechangia kiasi cha shilingi laki tano na kwamba ameahidi kuendelea kuchagiza zaidi katika kuleta maendeleo katika sekta ya elimu.

 

“Mimi kama  mbunge kitu kikubwa lengo langu kubwa ni kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo katika Nyanja mbali mbali lakini hasa katika sekta ya elimu na nichukua fursa hii ya kipeke kumshukuru Mama yetu mpendwa Rais Mama Samia Suluhu kwa kuweza kutupatia fedha  milioni 900 za madarasa ya uviko nah ii itaweza kuleta mapinduzi na mkombozi mkubwa kwa wanafunzi wetu kuweza kupata elimu bora kutona na miundombinu ya madarasa kuwa imara,”alisema Koka.

Katika hatua nyingine katika ziara hiyo Koka aliweza kuendelea kutoa sapoti katika sekta mbali mbali ambapo aliweza kuchangai kiasi cha shilingi tano kwa lengo la kuweza kuboresha zaidi miundombinu ya maji kwa wakazi wa mitaa mbali mbali iliyopo kata ya msangani ili waweze kuondokana na adha ya kutembea  umbari mrefu kufuata huduma ya maji safi na salama.

 

Kwa upande wake Diwani wa kata ya Msangani Denisi Mlowe alisema kwamba anafarijika sana kuona juhudi ambazo zinafanywa na Mbunge wa Kibaha mjini kwa vitendo  na kwamba wananchi wake bado kuna baaadhi ya maeneo wanakabiliwa na chanagomo ya huduma ya umeme na maji hivyo kunahitajika juhudi za makusudi ili kuwapelekea huduma hiyo.

 

Nao baadhi ya wananchi wa kata ya Msangani ambao waliweza kupata fursa ya kuhudhulia katika mkutano huo walimwomba Mbunge kuwasaidia kwa hali na mali upatikanaji wa maji na kuboresha zaidi huduma za kijamii ikiwemo katika suala zima la huduma ya afya pamoja na  masuala mbali ya miundombinu ya barabara ili ziweze kupitia kwa urahisi hasa katika kipindi cha mvua.

Ziara ya Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini Silvestry Koka katika kata ya Msangani imeweza kuibua  changamoto  pamoja na kero mbali mbali kutoka kwa wananchi ambazo ziliweza kujibiwa kwa ufasaha na kutolewa ufafanuzi wa kina kutoka kwa wakuu wa idara  pamoja na taasisi mbali mbali.

No comments:

Post a Comment

Pages