HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 13, 2021

NSSF yashiriki Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Kifedha Kitaifa, yatimiza malengo ya utoaji elimu ya hifadhi ya jamii

Waziri wa Nchi Afisi ya  Rais, Fedha na Mipango, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Jamal Kassim Ali (kushoto),    alipotembelea katika banda la Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) wakati wa  Maonesho ya Wiki ya Huduma za Fedha kitaifa yanayoendelea katika viwanja  vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam ambapo NSSF inaendelea kutoa elimu ya hifadhi ya jamii kwa sekta binafsi na sekta isiyo rasmi.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Masha Mshomba akipata maelezo kutoka kwa Afisa matekelezo Mwandamizi Hawa Godigodi, alipotembelea banda la NSSF wakati wa Maonesho  ya Wiki ya Huduma za Fedha kitaifa.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Masha Mshomba akielezea huduma mbalimbali zinazotelewa na NSSF katika maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa. Katika maadhimisho hayo NSSF inatoa elimu kuhusu hifadhi ya jamii, elimu kuhusu umuhimu wakujiwekea akiba, elimu ya  huduma zinazotolewa kwa njia  ya  mtandao ambapo ndio kipaumbele muhimu cha Mfuko pamoja na kueleza fursa za uwekezaji.
Mkurugenzi wa Idara ya Hifadhi ya Jamii, Ofisi ya Waziri Mkuu, Festo Fute (katikati) akisisitiza jambo alipotembelea banda la Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) wakati wa Maonesho ya Wiki ya Huduma za Fedha kitaifa katika viwanja  vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam, kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Masha Mshomba, kulia ni Meneja Uhusiano na Elimu kwa Umma, Lulu Mengele  pamoja na wafanyakazi wa  NSSF.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Dkt. John Mduma (kulia), akipata maelezo mbalimbali kuhusu ushiriki wa NSSF katika  Maonesho ya Wiki ya Huduma za  Fedha kitaifa. Maonesho hayo yanaendelea katika viwanja vya Mnazi mmoja, jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa  Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Masha Mshomba akitoa maelezo kwa Waziri wa Nchi Afisi ya  Rais, Fedha na Mipango, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Jamal Kassim Ali kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na NSSF wakati wa  Maonesho ya Wiki ya Huduma za Fedha kitaifa katika viwanja vya Mnazi mmoja.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko  Taifa wa Hifadhi ya Jamii  (NSSF), Masha Mshomba (wa kwanza mstari wa mbele)  akiwa katika ufunguzi wa Maonesho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi, Afisi ya  Rais Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Jamal K. Ali (aliyekaa katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Kamishna Uendelezaji wa Sekta ya Fedha kutoka Wizara ya Fedha Dkt. Charles Mwamwaja (kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Fatma Nyangasa na viongozi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa  wa Hifadhi  ya Jamii (NSSF), Masha Mshomba, akiwa katika maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa ambapo alipata fursa ya  kutembelea na kupata maelezo katika banda la Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi  (WCF) na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF). Mifuko hiyo ipo katika viwanja vya Mnazi mmoja kutoa elimu kuhusu  huduma mbalimbali zinazotolewa kwa wanachama wao.



Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umesema umefanikiwa kutimiza malengo yake ya utoaji ya elimu kuhusu hifadhi ya jamii, umuhimu wa kujiwekea akiba, huduma zinazotolewa kwa njia ya mtandao pamoja na kueleza fursa za uwekezaji kwa wanachama katika Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Kifedha Kitaifa yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Hayo yamesemwa jijini humo na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo, Masha Mshomba katika ufunguzi wa maadhimisho hayo ambapo amebainsha kuwa kufanikiwa kutoa elimu ya umuhimu wa hifadhi ya jamii kwa wateja na watu waliohudhuria katika banda lao.

" Tumetimiza malengo yetu ya kutoa elimu kwa wateja tumewaeleza wateja na wanachama umuhimu wa hifadhi ya jamii inavyomsaidia mtu anapostaafu au anapokosa uwezo wa kufanya kazi.

Mkurugenzi huyo amesema wametoa elimu ya umuhimu wa kuweka akiba kwa wanachama na wateja unavyoweza kuwasaidia siku za baadaye hasahasa wanaposhindwa kufanya, kustaafu na majanga.

Amesisitiza  kuwa mfuko huo si watu waliopo katika sekta rasmi hivyo hata watu wasio kwenye sekta hiyo wana fursa kujiunga na kuchangia kwani manufaa yake ni makubwa.

Amefafanua kuwa wateja na wanachama wamepewa elimu ya kuwekeza katika maeneo mengine ikiwemo fursa ya kuwekeza katika hatifungani hivyo wameelezwa kuchangamkia fursa hiyo. 

Akifungua maadhimisho hayo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango, Jamal Kassim Ali amesema Serikali imepanga kutumia fedha kwenye mitaji ya wajasiriamali wadogowadogo ambao wanatoa huduma za kifedha kwenye Mpango wa Maendeleo ya sekta ya Fedha hapa nchini.

Waziri huyo amaesema elimu ijikite kwenye huduma za Fedha ili waweze kukuza kipato cha mtu mmojamoja na kuongeza mapato kwa taifa hivyo ni vyema kujipima ipasavyo ili kuongeza ufanisi kwenye huduma za kifedha hapa nchini.

Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Kifedha Kitaifa yameanza Novemba 8 na yanatarajiwa kuhitimishwa Novemba 14 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

Pages