HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 13, 2021

Waziri Mkuu Majaliwa kufungua Kongamano la Biashara kati ya Tanzania na Uingereza

Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo akizungumza na waandishi wa habari (hawamo pichani,) juu ya Kongamano la Biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Uingereza litakalofanyika jijini Dar es Salaam.Hussein Ndubikile, Dar es Salaam.
Balozi wa Uingereza nchini Tanzania David William Concar akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Kongamano hilo baina ya Uingereza na Tanzania litakalofanyika Novemba 16 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
 
 

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anatarajia kufungua Kongamano la Biashara kati ya Tanzania na Uingereza litakalofanyika Novemba 16 mwaka huu katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere, Dar es Salaam.

Hayo yamesemwa leo jijini humo na Waziri wa Viwanda na Biashara Profesa Kitila Mkumbo wakati akizungumza na wanahabari kuhusu kongamano hilo.

Amesema kuwa kongamano hilo litafunguliwa na Waziri Mkuu Majaliwa na kuhudhuriwa na Mjumbe Maalumu wa Uingereza wa Masuala ya Biashara wa Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Lord Walney na kwamba washiriki takribani 200 kutoka Sekta Binafsi za nchi mbili watahudhuria huku wengine watashiriki kwa njia ya mtandao.

" Kongamano hili limeandaliwa kwa namna ya kipekee ili kuongeza tija ya matokeo tarajiwa ambapo limegawanyika katika makundi matatu yatakayofanya mijadala kwa wakati mmoja, yaani majadiliano kati ya Serikali ya Tanzania na ya Uingereza, baina ya sekta binafsi ya nchi hizo mbili pamoja na mdahalo kati ya Serikali na sekta hiyo," amesema Waziri Profesa Mkumbo.

Amebainisha kuwa kauli mbiu ya kongamano hilo ni Kuimarisha Ustawi Endelevu wa Kiuchumi kati ya Tanzania na Uingereza, hivyo litatoa fursa kwa washiriki kujadiliana kwa kina na kubaini fursa mpya za ushirikiano baina nchi hizo mbili.

Amesisitiza kuwa kupitia majadilainao hayo pande zote mbili zitaweza kupanua zaidi wigo wa ushirikiano katika maeneo ya biashara na uwekezaji hususan sekta za nishati, madini, miundombinu, kilimo, uchumi wa bluu na utalii.

Ameongeza kuwa kwa mujibu wa takwimu za Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) Nchi ya Uingereza ni ya pili kwa uwekezaji hapa nchini  ikiwa na miradi 945 yenye thamani ya Dola za Marekani 5.42 bilioni na kutoa ajira 275,384.

Pia amesema kuwa takwimu za Serikali ya Uingereza jumla ya thamani ya biashara baina ya nchi hizi mbili kwa mwaka 2021 ilikuwa pauni za Uingereza 156 milioni, huku nchi hiyo ikiuza hapa nchini bidhaa zenye thamani ya Pauni 127 milioni, na Tanzania ikiuza Uingereza bidhaa zenye thamani ya Pauni milioni 29.

Kwa upande wake, Balozi wa Uingereza nchini, David Concar amesema kongamano lina umuhimu kwa nchi zote kwani linakwenda kufungua fursa mpya za uwekezaji zilizopo.

Balozi huyo amesema katika kongamano hilo kutakuwa majadiliano baina ya Serikali ya Tanzania na UIngereza, sekta binafsi pamoja wawkilishi wa makampuni hivyo fursa mbalimbali za uwekezaji zitajadiliwa.

No comments:

Post a Comment

Pages