HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 07, 2021

Taasisi za kielimu za Kaizirege na Kemeboz zampongeza Rais Samia


Meneja wa shule za Kaizirege na Kemebos, Eurogius Katiti akitoa taarifa ya shule katika mahafali hayo.

 

Wahitimu wa kidato cha nne kwa shule ya sekondari Kaizirege na Kemebos.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi za Kaizirege na Kemebos, Yusto Kaizirege Ntagalinda.
 


Na Lydia Lugakila, Bukoba

Taasisi za kielimu za Kaizirege na Kemeboz zilizopo kata ya Ijuganyondo Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera zimempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suruhu Hassani kwa kuendelea kuimalisha mahusiano bora ya uwekezaji katika sekta binafsi.

Pongezi hizo zimetolewa na Meneja wa shule za Kaizirege na Kemebos Eurogius Katiti katika hotuba yake kwa Mgeni rasmi  katika mahafali ya 12 kwa Kaizirege shule ya msingi, mahafali ya ya 4 kwa shule ya msingi Kemebos yaliyofanyika shuleni hapo.

Akizungumzia tangu kuanzishwa kwa Taasisi hizo za kielimu Katiti amesema  hadi sasa taasisi hizo zimetimiza miaka 15  tangu zilipozinduliwa rasmi na Rais Mstaafu awamu ya nne Jakaya Mrisho Kikwete na kuwa tangu kipindi hicho hadi Leo wanaendelea kushuhudia kukua na kushuhudia taaluma bora na kupongeza serikali ya awamu ya 6 inayoongozwa na mhe, Rais Samia Suruhu Hassan ambayo imekuwa mdau mkubwa kwa kuimalisha mahusiano bora ya uwekezaji  katika sekta binafsi nchini kwani kwa asilimia kubwa taasisi hiyo imewezeshwa kiuchumi zaidi.

Amewapongeza pia wadau wengine walioshirikiana nao bega kwa bega ili kukuakwa taasisi hizo za Kielimu kuwa ni pamoja na mkurugenzi mtendaji wa Taasisi za Kaizirege na Kemebos Yusto Kaizirege Ntagalinda aliyeletwa wazo la kuanzisha shule na kuwa wazo lake lipewe heshima kwani amejenga msingi imara kwa vijana kwa kuwezesha kuwepo kwa wataalam wa baadae.

Katiti akizungumzia mafanikio ya taasisi hiyo amesema  wanapoadhimisha miaka 15 tangu kuanzishwa kwa taasisi ya Kaizirege na kuzaliwa taasisi mpya ya Kemebos kitaaluma zimekuwa kati ya shule bora kwani ki wilaya kimkoa na kitaifa zimeshika nafasi ya kwanza katika mitihani ya taifa mara kwa mara ikiwemo kuchukua tuzo ya Rais katika utunzaji mazingira na upandaji miti ikiwemo kupata tuzo kutoka wizara ya elimu sayansi na teknolojia na TAMISEMI kwa taaluma bora nchini.

Kufuatia hatua hiyo ya mafanikio kwa taasisi hizo Meneja wa shule hiyo amesema tayari mkurugenzi mtendaji wa taasi si hizo ameanzisha tuzo maalum kwa wanafunzi itakayowahusu wanafunzi watakaoweza kuingia kwenye  orodha ya wanafunzi 10 bora kitaifa na wale watakaoweza kuongoza kimasomo nafasi ya 1 hadi ya 5 kitaifa zawadi au tuzo itakuwa ni kusoma BURE ambapo tuzo hiyo imepewa jina la THE KAIZIREGE AND KEMEBOS ACADEMIC EXCELLENCY AWARD .

Aidha amewataka wanafunzi kuhakikisha wanapambania tuzo hiyo huku akiwaomba wazazi na walezi kutimiza majukumu kwa watoto wao ili wapate elimu bila vikwazo.

Akisoma lisala mmoja wa wahitimu hao wa kidato Cha nne Elen Katiti amesema kuwa kutokana na mikakati mbali mbali ya kusoma iliyobuniwa shuleni hapo na Meneja wa shule itawafanya wanapata matokeo mazuri katika mtihani wao wa mwezi  Novemba mwaka huu kwani wamenolewa vya kutosha.

Naye Mgeni rasmi katika mahafali hayo askofu mstaafu kutoka kanisa la Anglikana Jacton Rugumila amewahasa wazazi kuwalea watoto katika maadili mema na kuwaepusha na vishawishi mbali mbali.

Kwa upande wake muhitimu wa kidato Cha nne Kadija Jamal amewahimiza wahitimu wenzake kuendelea kuikamata elimu ikiwa ni pamoja na kujiadhali na anasa za kidunia na kutumia elimu hiyo kuwasaidia maishani mwao.

Jumla wa wahitimu 230 wa kidato cha nne wamehitimu huku darasa la saba wakihitimu wanafunzi 84


No comments:

Post a Comment

Pages