HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 11, 2021

Tamwa - Zanzibar kupigania ushiriki wa wanawake katika nafasi za uongozi


Mkurugenzi wa TAMWA-ZNZ Dkt. Mzuri Issa akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mkutano wa Chama hicho Tunguu Wilaya ya kati Unguja kueleza muhtasari wa ziara yao nchini Rwanda.


 Mkurugenzi wa TAMWA-ZNZ Dkt,Mzuri Issa (katikati) akiwa pamoja na Mkurugenzi wa ZAFELA Jamila Mahmoud pamoja na Mkurugenzi kutoka PEGAO Hafidh Abdi Said.

 

 

Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (Tamwa - Zanzibar) kitahakikisha ushiriki wa wanawake katika kupigania nafasi za uongozi hasa katika vyombo kutunga sheria inaongezeka Zanzibar na Tanzania.

 

 

Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake TAMWA-ZNZ Dkt. Mzuri Issa aliyasema hayo leo katika ofisi za Chama hicho zilizopo Tunguu Wilaya ya kati Unguja.

 

“Katika kupanga mikakati ya kuongeza nafasi za wanawake lazima tuiangalie nchi  ya Rwanda kwa kuwa ndio nchi pekee kwa Africa iliopiga hatua kubwa zaidi ya ushiriki wa wanawake kwenye nafasi za uongozi iwe wa kiserikali na hata taasisi binafsi” alieleza Dkt. Mzuri.

 

Dkt. Aliyaeleza mara baada ya kurejea Rwanda ambako alikuwa na ziara ya kikazi akiwa na ujumbe  wengine kutoka taasisi za ZAFELA pamoja na PEGAO kurudi ambako walijifunza mengi katika kuongeza nafasi za wanawake Serikalini na Binfsi.

 

Alisema kwa kuwa Rwanda ni kiongozi wa dunia kwenye masuala ya uwakilishi wa wanawake katika nafasi za uongozi, ipo sababu kwa  Serikali zetu kujifunza kutoka kwao sambamba na jamii pia kuona wanawake wengi walivyo na anafasi kubwa katika muundo wa Serikali na asasi za kiraia.

 

Akifafanua zaidi alisema nchi ya Rwanda  kwenye Bunge lao la kutunga sheria wanawake ni asilimia 61 idadi kubwa zaidi kuliko wanaume na nchi yao inapiga hatua zaidi kimaendeleo kila leo.

 

Sambamba na hayo akiendelea kufafanua zaidi alisema kwa mfano Baraza la Mawaziri Nchini Rwanda  lina asilimia 53. Baraza la Wilaya ni asilimia 41, kwenye sekta ni asilimia 42.

 

Alisema kutokana na mazingira hayo Zanzibar ambayo ni sehemu ya Tanzania pia imeridhia mikataba mbali mbali inayosisitiza usawa wa kijinsia ikiwemo ya Beijing Platform of Action ya 1995, CEDAW, SADC na Itifaki ya AU zinazosisitiza usawa wa wanawake na wanaume katika ngazi za maamuzi ina kila sababu ya kuzingatia suaala la usawa wa kijinsia katika uongozi.

 

Aidha  alisema licha ya changamoto mbali mbali zinazoendelea kuwakabili wanawake wengi hadi sasa Zanzibar ina asilimia 40 ya uwakilishi wa viti maalum kama inayoelezwa kwenye katiba ya Zanzibar kupitia marekebisho yake 2010.

 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Jumuia ya Wanaseheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA) Jamila Mahmoud alisema upigaji wa hatua kwa Rwanda na wanawake wengi kushika nafasi za uongozi ni mazingira yanayotokana na utiiji wa sharia kwa wananchi wake.

No comments:

Post a Comment

Pages