HABARI MSETO (HEADER)


January 28, 2022

MRITHI WA MAALIM SEIF KUPATIKANA KESHO

Chama cha ACT Wazalendo kesho Januari 29, 2022 kitafanya Mkutano Mkuu Maalum kwa kuchagua viongozi  watakaokiongoza chama hicho.

Moja ya nafasi hizo ni ya Mwenyekiti wa chama Taifa iliyoachwa wazi na Marehemu Maalim Seif Sharif Hamad aliyefariki dunia Februari 17, 2021.

Nafasi nyingine ni ya Makamu Mwenyekiti pamoja na nafasi moja ya Halmashauri Kuu ya Taifa.

Mgeni rasmi wa Mkutano huo ni Kiongozi wa chama kikuu cha Upinzani nchini Zimbabwe cha Citizen Coalition for Change (CCC), Ndugu Nelson Chamisa.

No comments:

Post a Comment

Pages