Chama cha ACT Wazalendo leo Januari 29, 2022 kinafanya Mkutano Mkuu Maalum kwa kuchagua viongozi watakaokiongoza chama hicho.
Moja
ya nafasi hizo ni Mwenyekiti wa chama Taifa iliyoachwa wazi na
Marehemu Maalim Seif Sharif Hamad aliyefariki dunia Februari 17, 2021.
Nafasi nyingine ni Makamu Mwenyekiti pamoja na nafasi moja ya Halmashauri Kuu ya Taifa.
Mgeni
rasmi wa Mkutano huo ni Kiongozi wa chama kikuu cha Upinzani nchini
Zimbabwe cha Citizen Coalition for Change (CCC), Ndugu Nelson Chamisa.
Mwenyekiti wa Ngome wa Vijana Abdul Nondo, akiwa katika ukumbi wa mkutano Mkuu Maalum wa Chama cha ACT Wazalendo leo Januari 29, 2022 jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wajumbe wa mkutano Mkuu Maalum.
Baadhi ya wajumbe wa mkutano Mkuu Maalum wa Chama cha ACT Wazalendo wakiwa ukumbini.
No comments:
Post a Comment