MENEJA
mgodi wa dhahabu wa North Mara inaomikikiwa kwa pamoja na Kampuni ya
Barrick na Serikali ya Tanzania, Georgia Mutagahywa amesema ofisi yake
haihusiki na uchafuzi wa maji ya Mto Mara.
Taarifa
ya Uongozi wa mgodi wa Dhahabu wa North Mara unaomilikiwa kwa pamoja na
Kampuni ya Barrick na Serikali ya Tanzania umekana kuhusika na uchafuzi
wa maji ya mto Mara.
Uongozi
wa mgodi huo ulilazimika kutoa taarifa hiyo hivi karibuni baada ya
kuwepo kwa uchafuzi wa maji katika mto Mara ukihusisha kemikali ya
Zebaki.
Kwa mujibu wa
taarifa hiyo, mgodi huo upo mbali zaidi ya kilometa 85 pia Zebaki si
sehemu ya orodha ya vitendanishi vya mgodi wao hivyo basi Zebaki
inayohisiwa kuwemo mto Mara haitoki kwenye mgodi huo.
Mutagahywa
amesema Mamlaka ya Bonde la Maji ya Ziwa Victoria mara kwa mara
huchukua sampuli za maji katika maeneo yaliyo jirani na migodi na mgodi
wenyewe una mpango madhubuti wa ufuatiliaji wa maji ya ardhini na
hakuna ushahidi wa kuwepo zebaki au uchafu mwingine wowote kwenye maji
ndani au karibu na maeneo ya uzalishaji.
"Lakini
pia serikali iliunda timu ya wataalamu inayoongozwa na Baraza la Taifa
la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) ambayo imefanyakazi kwa karibu na Mgodi
wa Dhahabu wa North Mara ili kuhakikisha hakuna uchafuzi wa mazingira
au maji unaotokea katika mgodi huo na katika maeneo yanayouzunguka,"
ilisomeka sehemu ya taarifa hiyo iliyotolewa na Mutagahywa.
Imebainisha
pia mgodi huo umefikia lengo muhimu la uhifadhi wa taka zitokanazo a
mchakato wa uchenjuaji wa madini kwa kupunguza kiasi cha maji
yaliyohifadhiwa kwa kiasi kikubwa kutoka mita za ujazo milioni saba hadi
mita za ujazo 800,000 ndani ya kipindi cha miaka miwili, kama
ilivyokubaliwa katika Mkataba wa Maelewano na NEMC.
“Hayo
ni mafanikio makubwa, ambayo yanaonesha zaidi dhamira na jitihada za
Mgodi wa Dhahabu wa North Mara zinakwenda sambamba kwa kuhakikisha
hakuna uchafuzi wa maji au mazingira kwenye Mgodi na maeneo
yanayouzunguka,” ilihitimisha hivyo taarifa hiyo.
No comments:
Post a Comment