Afisa
mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB,
Filbert Mponzi (kushoto) akizindua rasmi Bima mpya ya UMEBIMA, wakati
wa hafla fupi ya uzinduzi huo iliyofanyika katika viwanja vya Soko la
Karume Ilala jijini Dar es Salaam, jana, Katikati ni Afisa Mtendaji Mkuu
wa Jubilee Life, Hellen Mzela na kulia ni Mkuu
wa Idara ya Bima NMB, Martine Massawe.
Na Mwandishi Wetu
Benki ya NMB yazindua msimu wa pili wa
‘Umebima’ ikiwa ni kampeni ya kuhamamisha na kuelimisha matumizi ya
huduma za Bima kwa Wateja wake na Watanzania wote kwa ujumla.
Kampeni
hii ilizinduliwa katika Soko la Karume na Afisa Mkuu wa Wateja binafsi
na biashara wa NMB, Filbert Mponzi akishirikiana na Mkuu wa idara ya
Bima wa NMB, Martin Massawe ikilenga kuongeza uelewa wa huduma za bima
nchi kote sambamba na kupata Wateja wapya wa huduma hiyo.
Afisa
Mkuu kitengo cha Wateja binafsi wa NMB, Filbert Mponzi alisema licha ya
elimu juu ya bima kuongezeka, bado kuna watanzania wengi hawatumii
huduma hizi. Takwimu zinaonesha ni asilimia 15 tu ya watanzania
wanaotumia huduma mbalimbali za Bima.
Benki
ya NMB inazo huduma tofauti za Bima inazoshirikiana na kampuni tofauti
za Bima ambazo zinapatikana kwenye matawi 226 ya NMB nchini kote,
mtandaoni kupitia Mkononi plus Kwa piga *150*68# au popote pale ulipo
mpaka mahali ambako kampuni za Bima hazijafika.
Bima zinatolewa na Benki ya NMB ni Bima ya ujenzi, Afya, kilimo, Chombo cha moto, maisha, Mali n.k
Benki
ya NMB imeshirikiana na kampuni zinazoaminika nchini ambazo ni Sanlam
Life, Shirima la Bima la Taifa(NIC), Jubilee insurance, Jubilee life,
Metropolitan life, Britain Insurance na shirima la Bima Zanzibar(ZIC)
hivyo inauhakika ya kukidhi mahitaji yote ya wateja.


No comments:
Post a Comment