MKUU
wa Mkoa wa Tanga, Adam Malima leo Jumatano Machi 16, 2022 ametembelea
eneo la ajali iliyotokea jana usiku wilayani Handeni na kuua watu wanne.
Akiwa katika eneo la ajali, RC Malima amezungumza na baadhi ya watu walioshuhudia ajali hiyo.
Baadhi
ya mashuhuda walioshuhudia ajali hiyo, wamemueleza RC Malima kuwa
ilitokea baada ya gari aina ya Costa iliyokuwa na abiria ikitokea
Korogwe kuelekea Handeni kugonga baadhi ya wananchi waliokuwa wakisaidia
kuziba pancha kwenye hiace iliyokuwa imepaki pembeni ya barabara.
"Hiace
ilikuwa 'imeburst' kulikuwa na wanakijiji wanasaidia kubadilisha tairi,
wakati costa inakuja akawa anaelekezwa asimame lakini kwa sababu
haikuwa na taa ikagonga wale wanakijiji waliokuwa wanasaidia na kuanguka
huko bondeni, kwa hiyo waliopata ajali wengi ni wananchi," amesema
shuhuda huyo.
RC
aliongozana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Safia Jongo. Majeruhi wa
ajali hiyo wamelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Handeni wakiendelea
na matibabu.
No comments:
Post a Comment