HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 17, 2022

Washindi 100 wa droo ya 10 NMB MastaBata wapatikana

 

Meneja Mwandamizi Kitengo cha Kadi Benki ya NMB, Manfred Kayala, akibonyeza kitufe cha kompyuta kumtafuta mmoja kati ya washindi 100 wa droo ya 10 ya Kampeni ya ‘NMB MastaBata Kivyako Vyako’ iliyofanyika leo Machi 17, 2022 jijini Dar es Salaam. Kulia ni Ofisa Huduma kwa Wateja NMB, Suzan Manga na kushoto ni Msimamizi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), Irene Kawili. (Na Mpiga Picha Wetu).


Meneja Mwandamizi Kitengo cha Kadi Benki ya NMB, Manfred Kayala, akionesha kadi na mashine ya malipo wakati wa kuchezesha droo ya 10 ya Kampeni ya NMB MastaBata Kivyakovyako’ iliyochezeshwa jijini Dar es Salaam leo Machi 17 jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mwakilishi kutoka Bodi a Michezo ya Kubahatisha (GBT), Irene Kawilis na kulia ni Ofisa Huduma kwa wateja, Suzan Manga. (Na Mpiga Picha Wetu).

 

Na Mwandishi Wetu


DROO ya wiki ya mwisho ya msimu wa tatu wa Kampeni ya ‘NMB MastaBata Kivyako Vyako’ inayoendeshwa na Benki ya NMB, ikilenga kuhamasisha matumizi ya kadi badala ya pesa taslimu imefanyika jijini Dar es Salaam leo, ambapo washindi 100 wamepatikana na hivyo kufanya jumla ya washindi waliozawadiwa kufikia 950. 

 

Washindi hao 100 walijinyakulia kiasi cha Sh. Mil. 10 (sawa na Sh. 100,000 kila mmoja), ambazo zinafanya zawadi za pesa zilizotolewa hadi sasa kufikia Sh. Mil. 150 kati ya Sh. Mil. 240 zinazoshindaniwa.

Meneja Mwandamizi wa Kitengo cha Kadi wa NMB, Manfredy Kayala, alisema kumekuwa na mafanikio makubwa katika uhamasishaji wa matumizi yasiyohusisha pesa taslimu na kuwataka wateja kuendelea kutumia kadi zao na Vituo vya Mauzo (PoS), ili kujiongezea nafasi ya kushinda katika fainali. 

 

Droo hiyo iliyofanyika Makao Makuu ya NMB, Mtaa wa Ohio jijini Dar es Salaam, ilichezeshwa chini ya uangalizi wa Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), Irene Kawili, ambaye aliwahakikishia wateja kuwa washindi hupatikana kwa njia halali na kwamba vigezo na masharti vinazingatiwa.

 

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma, Fatma Hassan Toufiq, amefanikiwa kuwa miongoni mwa washindi 100 wa droo ya 10 ya msimu wa tatu wa Kampeni ya ‘NMB MastaBata Kivyako Vyako’ inayoendeshwa na Benki ya NMB, ikilenga kuhamasisha matumizi ya kadi badala ya pesa taslimu na alikiri kwamba yeye ni mteja wa muda mrefu wa NMB, na kwamba kwa kipindi chote hicho amekuwa ‘Balozi Mwema’ wa benki hiyo - miongoni mwa jamii inayomzunguka, wakiwemo wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anaoshirikiano nao.

 

Kujiweka kwenye nafasi ya kushinda droo ya mwisho ya ‘Grand Finale’ ni rahisi, endelea kutumia NMB Mastercard kufanya malipo mtandaoni, kwa QR code au POS na unaweza kujiweka kwenye nafasi nzuri yakuingia kwenye droo.

No comments:

Post a Comment

Pages