Huduma hiyo ya malipo ya kimataifa inayojulikana kama Kadi ya Popote Visa ni matokea ya ushirikiano kati ya TCB na Visa International ya Marekani inayoongoza duniani katika teknolojia bunifu za malipo ya kidijitali.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wake jijini Dar es Salaam, Afisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo, Bw Sabasaba Moshingi alisema Popote Visa Card ina uwezo wa hali ya juu kusaidia kutimiza ndoto za taasisi hiyo ya kuendeleza huduma jumuisha za kifedha nchini.
TCB na mshirika wake wameazimia kuunga mkono juhudi za kitaifa za kujenda uchumi wenye matumizi madogo ya fedha taslimu kwa kuwekeza katika suluhisho bunifu za malipo ya kidijitali ambazo ni rahisi zaidi, salama na zinazozingatia ufanisi wa usimamizi wa fedha.
“Huduma kama kadi ya malipo ya kimataifa tuliyozindua leo na ushirikiano wetu na kampuni ya Visa ni muhimu sana katika juhudi za serikali kujenga uchumi wa kidijitali na kuifanya Tanzania kuwa taifa lisilotegemea sana malipo yanayofanywa kwa fedha taslimu,” Bw Moshingi alibainisha.
Aliwaambia waandishi wa habari kuwa uamuzi wa TCB kushirikiana na Visa unatokana na kampuni hiyo kuwa kigogo wa teknolojia za malipo duniani ikiwa na mtandao wa wafanyabiashara milioni 61 wa kimataifa.
Wakizungumza wakati wa uzindunzi huo, maafisa waandamizi wa Visa Afrika Mashariki, walisema dhamira ya kampuzi hiyo si tu kuongeza matumizi ya kadi za kidijitali nchini peke yake bali duniani kote kuwahudumia wananchi, wafanyabiashara na serikali mbalimbali.
Makamu wa Rais wa Visa na Mkurugenzi Mtendaji wake wa Afrika Mashariki, Bi Corine Mbiaketcha Nana, alisema Tanzania ina kila kitu kinachohitajika kuwa uchumi wa kisasa zaidi wa kidijitali.
“Kama suluhisho zote bunifu za malipo ya kidijitali, matumizi ya Popote Visa Card yana manufaa mengi na faida kubwa kwa watu binafsi, mashirika na serikali,” Bi Nana alifafanua na kusisitiza kuwa mchango wake mkubwa hasa kwa wananchi wa kawaida ni maendeleo ya huduma jumuishi za kifedha.
Uzinduzi wa UCB Popote Visa Card umefanyika wiki mbili bada ya serikali kutangaza mipango na uwekezaji wake kwenye ujenzi wa uchumi usiotegemea sana fedha taslimu kupitia Mpango wa Tanzania ya Kidijitali.
Kwa mujibu wa Waziri wa TEHAMA, Bw Nape Mnauye, hivi karibuni Tanzania ilipata mkpo nafuu kutoka Benki ya Dunia kwa ajili ya utekelezaji wa azma hiyo wenye thamani ya dola za kimarekani milioni 150.
Makamu wa Rais wa VISA card Africa Mashariki Corine Nana (katikati) pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Sasabasa Moshingi wa pili kushoto wakionesha mfano wa POPOTE VISA CARD wakati wa uzinduzi rasmi wa kadi hiyo iliyozinduliwa na Tanzania Commercial Bank wengine pichani ni pamoja na Mkurugenzi wa Teknohama wa Tanzania Commercial Bank Jema Mssuya, Mkurugenzi Mtendaji wa UBX Tanzania LTD, Seronga pamoja na Meneja Mwandamizi wa Intanet Baking wa TCB Allen Manzi hafla hiyo imefanyika leo jijini Dar es Saam.
No comments:
Post a Comment