Na Mwandishi Wetu
SERIKALI
imewataka wataalamu wanaoandaa muundo wa mitaala nchini kuhakikisha
wanakidhi matamanio ya Watanzania ya kuwa na mitaala mipya ya elimu
nchini kuanzia ngazi ya Awali, Elimu Msingi, Sekondari na Ualimu.
Hayo
yamesemwa leo Machi,23, 2022 na Naibu Katibu Mkuu (Elimu) Wizara ya
Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Carolyne Nombo katika mazungumzo
yake na wataalamu wanaoendelea na kazi ya uandaaji wa muundo wa mtaala.
Amesema kazi hiyo ni muhimu hivyo amewaomba waifanye kwa weledi na umakini.
"Serikali
inawategemea mmalize kazi hii kwa wakati na weledi na mitaala mipya
ianze kutumika kama ilivyokusudiwa" amesema Profesa Nombo.
Kazi
ya uandaaji wa muundo wa mitaala inaendelea kufanyika Mjini Morogoro
kuanzia Machi 21, 2022 ikiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati Wataalam
(Technical Commitee) inayosimamia kazi ya maboresho ya Mitaala Profesa
Makenya Maboko na wajumbe kutoka vyuo vikuu, Wizara ya Elimu, Sayansi na
Teknolojia, Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Taasisi ya Elimu Zanzibar
(TEZ) na wataalam kutoka sekta binafsi.
No comments:
Post a Comment