Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) limepongezwa kwa juhudi kubwa inazofanya za kutangaza vivutio vya utalii.
Pongezi hizo zimetolewa leo na Waziri wa viwanda, biashara na uwekezaji Mhe.Dkt. Ashatu Kijaji alipotembelea banda la TANAPA wakati akifungua rasmi maonyesho ya 9 ya biashara yanayofanyika jijini Tanga.
Maonyesho haya yanaendelea hadi tarehe 6/6/2022.
Sekta mbalimbali, mashirika ya serikali na binafsi yanashiriki kwenye maonyesho haya.
Pia, Mkuu wa mkoa wa Tanga Mhe. Adam Malima amehudhuria ufunguzi wa maonyesho ya 9 ya biashara katika jjiji la Tanga.
No comments:
Post a Comment