Mtafiti Emmanuel Mtoto akielezea namna wanawake wanavyoshiriki katika usimamizi wa rasilimali misitu.
Afisa Kujengea Uwezo kutoka Katika Shirika la Kuhifadhi Misitu Asili Tanzania, Simon Lugazo akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mafanikio ya tafiti.
Na Mwandishi Wetu, Morogoro
WANAWAKE
wanaoishi katika jamii zenye uhifadhi simamizi shirikishi wa misitu
wameonesha mabadiliko makubwa katika ushiriki, usimamizi na utumiaji wa
rasilimali hizo.
Hayo
yamesemwa na Ofisa Muhahamsishaji wa Shirika la Kuhifadhi Misitu ya
Asili Tanzania (TFCG), Saimon Lugazo wakati wa warsha iliyohusisha asasi
mbalimba zinazojishughulisha na rasilimali misitu ambazo ni mwanachama
wa Chama Cha Wafanyakazi za Misitu Tanzania (TFWG).
Lugazo
alisema bado hakujakuwa na idadi ya sawa kati ya wanaume na wanawake,
ila ni wazi kuwa wanawake wameamka hasa kwenye suala la umiliki wa
ardhi, kufanya biashara za misitu na kushiriki katika vikundi vya hisa.
Kwa
upande wake Dk.Mroto ambaye amehusika na utafiti alisema wapo wanawake
ambao kwa sasa wameanza kujishughulisha na ukataji mkaa na kuwaweza
kufungua miradi mbalimbali huku akishauri pia vijana nao wanahamasishwe
vya kutosha kushiriki katika mradi.
Nao
baadhi ya washiriki wa warsha hiyo akiwemo Marygoreth Lwekiza kutoka
Shirika la Mpingo na Mandeleo (MCDI), Fadhila Kateta kutoka Jumuiko la
Maliasili Tanzania na Isaya Sekibo kutoka Suredo wamesema kuwa miongoni
mwa shughuli kubwa wanazozifanya ni kuhakikisha wanawake wanashirikishwa
na wanashiriki vya kutoka katika shughuli za misitu.
Warsha
hiyo ambayo imehusisha wanachama TFWG imewezeshwa na Mradi wa Kuhifadhi
Misitu kupitia Biashara Endelevu ya Mazao ya Misitu (CoFoReST )
unaoendeshwa na TFCG wakishirikiana na Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa
Misitu Tanzania (MJUMITA) kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Uswizi
(SDC).
No comments:
Post a Comment