HABARI MSETO (HEADER)


 


Breaking

July 24, 2022

BAJAJI, BODABODA ZISITUMIKE KATIKA VITENDO VYA KIHALIFU-RAIS SAMIA

 


NA JASMINE SHAMWEPU, DODOMA


RAIS wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Samia Suluhu Hassan amewataka Maafisa usafirishaji kutotumika kwenye vitendo vya kihalifu kwani usafiri wa Bajaji na Bodaboda ni sekta ya usafiri wa wanyonge tena wa bei nafuu.

Akizungumza kwa njia ya simu katika kongamano la Madereva wa Bodaboda na Bajaji Mkoa wa Dodoma kongamano Mahususi kwa ajili ya kuimarisha ushiriki wa Madereva wa Bodaboda na Bajaji katika Sensa ya Watu na makazi Rais Samia Alisema kumekuwa na tabia mbaya ya baadhi ya Madereva Bodaboda kutumika kwenye ujambazi.

"Kesi za Bodaboda kukwapua mikoba ya akinamama zimekuwa nyingi kiasi kwamba tabia hii ikiendelea mtaharibu huduma yenu ambayo imeonekana kimbilio kubwa la wanyonge,"

Na kuongeza kuwa "Nipo pamoja na nyinyi ahikisheni mnakwenda kuhamasisha watu kushiriki katika zoezi la Sensa ya Watu na makazi lakini pia nipo tayari kusikikiza kero zenu Mkuu wa mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka atanifikishia kero zenu,"Alisema  

Awali akimueleza Rais samia lengo la kongamano hilo Mkuu wa mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka Alisema Kongamano hilo limewakutanisha Madereva wa Bodaboda na Bajaji wa mkoa wa Dodoma ambapo kila mkoa wametoka wawakikishi wawili na mkoa umetoa wawakikishi 30 kwa kila wilaya lakini pia ofisi ya mtawimu Mkuu wa serikali ndio iliyofanikisha kongano hilo.

Kwa Upande wake Mtakwimu Mkuu Dkt Albina akiongea katika kongamano hilo alieleza kuwa wamekusanyika ili kuwaendelea Kuhamasisha umuhimu wa  zoezi kubwa la Sensa ya Watu na makazi inayotarajiwa kufanyika Agosti 23 mwaka huu.

"Hii ni Sensa ya 6 na sensa ya mwaka huu ni ya kipekee na tofauti kwani zoezi zima la kuhesabu litakuwa la kidigitali na Niwatoe hofu zoezi la Sensa ni hitaji la kisheria na sio hiyari hivyo sote tuhakikishe tunashiriki ili taifa iweze kupata takwimu sahihi na kwa maendelea pia ,"Alisema Dkt Albina.

Na kuongeza"Tuchukue ujumbe wa leo na mkausambaze katika vituo vyenu na kwa abiria wenu umuhimu ifikapo 23 mwezi Agosti Tukumbuke kuwa  kwenda kuhesabiwa inalifanya taifa kutupangia  Maendeleo yetu Wananchi wake," Alisema Dkt Albina.

No comments:

Post a Comment

Pages