Makamu Mkuu wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini anayeshughulikia Taaluma, Utafiti na Ushauri Elekezi, Profesa Provident Dimoso akimpatia maelezo mteja aliyetembelea katika banda la Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini katika Maonesho ya vyuo vya Elimu ya Juu jijini Dar es Salaam.
Na Asha Mwakyonde, Dar es Salaam
MAKAMU Mkuu wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini anayeshughulikia Taaluma, Utafiti na Ushauri Elekezi, Profesa Provident Dimoso amesema kuwa chuo hicho kina tatua changamoto za ajira kwani kimeanzisha kituo cha Ubunifu na Ujasiriamali kwa wanafunzi wote wanaosoma katika chuo hicho.
Pia amewakaribisha wahitimu wa kidato cha nne kwa ajili ya kujiunga na masomo ya ngazi ya chati na waliomaliza kidato cha sita kujiunga ngazi ya Shahada 'degree' pamoja na wale ambao ufaulu wao ni wa alama moja ' Principal Pass' nao wanaweza kujiunga na chuo hicho kwa ngazi ya diploma.
Akizungimza Julai 22,2022 katika banda la Chuo hicho kwenye Maonesho ya Vyuo vya Elimu Juu yaliyoandaliwa na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania ( TCU) katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam Prof. Dimoso amesema kuwa wana kozi zote zinazohusuana na masuala ya mipango kuanzia ngazi ya cheti.
Prof. Dimoso ameeleza kuwa ili mwanafunzi ajiunge na chuo hicho ngazi ya cheti anatakiwa awe na ufaulu wa alama D nne na kwamba kinatoa kozi za Shahada 'degree' ili mwanafunzi aweza kujiunga lazima awe na cheti ' Certificate' kutoka chuo kinachotambuliwa na serikali Kwa kuwa na ufaulu Wastani wa Alama za Daraja (GPA), ya 2 au awe amemaliza kidato cha sita na kupata ufaulu wa alama 1.
" Imekuwa ni utamaduni kwa Watanzania kudhani kwamba ukimaliza kidato cha sita na ukapata alama moja ya ufaulu wanadhani wamefeli mwanafunzi anaweza kuendelea na masomo kwa kusoma masomo ya diploma ya chuo hiki," amesema Prof. Dimoso.
Amefafanua kuwa mwanafunzi anapotoka diploma ana nafasi kubwa ya kusoma Shahada kwa aliyepata GPA ya 3 na kwa wale ambao wamemaliza kidato cha sita na kupata alama 2 naye ana uwezo wa kusoma Shahada.
Prof. Dimoso ameongeza chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini kinatambuliwa na TCU na kina usajili wa Baraza la elimu na mafunzo ya ufundi (NACTEVET), hivyo mwanafunzi anaposoma Shahada katika chuo hicho uzito wake ni sawa na kusoma chuo chochote duniani kwa kuwa ni kizuri,kina ubora na kimejikita kwenye masuala ya mipango.
Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini kinamilikiwa na serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango na kimeanzishwa kwa sheria Namba 8 ya mwaka 1980 ya Bunge la Tanzania ambayo kimeipa chuo hicho majukumu matatu ya kufundisha, kufanya utafiti na kutoa ushauri elekezi.





No comments:
Post a Comment