Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Dkt. Asha-Rose Migiro leo Julai 25, 2022 ametembelea kambi ya wanamichezo wa Tanzania wataoshiriki kwenye Michezo ya 22 ya Jumuiya ya Madola iliyopangwa kuanza Julai 28, 2022, na kuwatakia kila la heri kwenye michuano hiyo inayoshirikisha jumla ya nchi 72.
Dkt.
Migiro, ambaye alimuwakilisha kiongozi wa msafara Waziri wa Utamaduni,
Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa katika hafla ya kukaribisha
rasmi nchi zinazoshiriki, alitoa pia salamu za Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa wanamichezo hao,
akisema kiongozi huyo wa nchi na Watanzania wote kwa ujumla wana imani
kubwa na wanamichezo hao kwamba watafanya vizuri kwenye mashindano.
"Macho
na masikio ya Mhe. Rais na ya Watanzania wote yako hapa Birmingham na
wote wanawategemea kwamba mtafanya vyema kwenye michezo hiyo hivyo
mjitume na kupigania heshima ya nchi kwa nguvu zote, huku mkidumisha
amani, nidhamu na furaha wakati wote mtaokuwa hapa", alisema.
Kwenye
michezo hiyo Tanzania inawakilishwa na wanariadha tisa, mabondia
watatu, wacheza judo wawili na waogeleaji wawili. Wachezaji wote
wameshawasili Birmingham isipokuwa wanariadha wa marathon ambao walikuwa
kambini Arusha na wanatarajiwa kuwasili siku tatu kabla ya michuano
kuanza.
Balozi
wa Tanzania nchini Uingereza Dkt. Asha-Rose Migiro akifurahia zawadi
zilizoandaliwa na wanamichezo wa Tanzania kwenye Michezo ya Jumuiya ya
Madola alipowatembelea katika kijiji cha wanamichezo katika Chuo Kikuu
cha Birmingham leo Jumatatu Julai 25, 2025.






No comments:
Post a Comment