Serikali
imeviasa Vyuo Vikuu Nchini viingie ushirikiano na Vyuo Vikuu vya nje
ili kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali kuboresha sekta ya elimu
iendane na mahitaji ya soko la ajira la ndani na nje.
Hayo
yamesemwa na Katibu Mkuu a Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknoloja Dkt.
Francis Michael katika Kilele cha Maonesho ya 17 ya Elimu ya Juu,
Sayansi na Teknolojia yaliyoandaliwa na Tume ya Vyuo Vikuu Nchini (TCU)
katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.
Amesema
kuwa vyuo vikishirikiana na vyuo vya nje vitasaidia kukuza sekta ya
elimu kwa kubadilshana uzoefu wa jinsi kuviendesha hali itakayosababisha
vyuo vya nje kuwekeza hapa nchini.
" Naviasa
vyuo vya ndani viingie link na vyuo vya nje kuendelea kuboresha sekta ya
elimu hata vya nje vije kuwekeza Tanzania," amesema Dkt. Michael.
Amebainisha
kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inaendelea kufanya kwenye ya sekta ya
elimu ikiwemo kuimarisha udhibiti ubora wa vyuo vikuu, kuhakikisha
programu za masomo zina wahadhiri wenye sifa na miundombinu, kutenga
fedha za udhibiti ubora pamoja na kuongeza ufadhili wa fedha za mikopo.
Amesisitiza
kuwa katika kuendelea kuboresha sekta ya elimu ikiwemo kutenga Sh
Bilioni 6.4 za udhibiti ubora wa mifumo na mitaala pamoja na kuongeza
fedha za mikopo Sh Bilioni 573.
Ametoa wito kwa
vyuo vikuu vinavyodahili wanafunzi kufuata sheria na utaratibu za
udahaili ili kuepuka kuwasababishia hasara waombaji wa nafasi za masomo
na kwamba vitakavyokiuka Serikali itavichukulia hatua za kisheria.
Kwa
upande wake, Mwenyekiti wa TCU, Profesa Penina Mlama amesema kuwa tume
hiyo itaendelea kuboresha mifumo ya udhibiti ubora wa ndani na
kuishukuru wizara hiyo kwa ushauri unaoisaidia kutekeleza majukumu yake
kikamilifu.
Amewashukuru wananchi na washiriki
kwa kushiriki maonesho hayo na kuongeza kuwa yametoa fursa kwa vyuo
vikuu na taasisi shiriki kujitangaza na kuimarisha mahusiano.
Nae
Katibu Mtendaji wa tume hiyo, Profesa Chares Kihampa amesema kuwa jumla
ya taasisi 75 zimeshiriki maonesho ya mwaka hivyo wataendelea
kushirikiana na vyuo vikuu ili kutimiza malengo ya Serikali ya kutoa
elimu.
Makamu Mwenyekiti wa Chuo Kikuu cha
Kilimo cha Sokoine (SUA), ambaye pia ni Mwakilishi wa Washiriki, Raphael
Chibunda ameipongeza TCU kwa kuendelea kuanadaa maonesho kwani
wamefaidika kuongeza idadi ya waombaji kutoka 6,000 kufikia 13,000.
Ameishukuru
wizara kwa kuweka msukumo kwenye maonesho pamoja na kuishauri TCU
kuvialika vyuo vya Bara la Afrika kuja kushiriki.




No comments:
Post a Comment