HABARI MSETO (HEADER)


 


Breaking

July 27, 2022

LATRA yapiga marufuku mahubiri, biashara katika mabasi

 


 

Na Jasmine Shamwepu, Dodoma


MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA ), CPA Habibu Suluo, amepiga marufuku mahubiri , biashara, mziki mkubwa na picha zisizo na Maadili kufanyika ndani ya mabasi makubwa yanayofanya safari zake mikoani.


Pia Mkurugenzi huyo ametoa rai kwa abiria kutoa taarifa mapema endapo gari au waliopanda inaruhusu huduma hizo Kuendelea ndani ya basi huku safari ikiwa inaendelea .


Akiongea na waandishi wa habari leo Wakati wa utekekezaji wa shughuli za mamlaka ya udhibiti usafiri ardhini LATRA na muelekeo wa utekekezaji kwa mwaka w fedha 2022/2023.


Amesema kumekuwa na baadhi ya vyombo hivyo kukiuka miiko ya usafirishaji na kutoa rai kwa abiria kutoa taarifa mapema endapo gari walilopanda linaruhusu huduma hizo kuendelea ndani ya basi huku safari ikiwa inaendelea.


Mkurugenzi huyo alisema  huduma hizo ndani ya mabasi ni marufuku kufanyika kwani zimekuwa zikileta hisia tofauti kwa sababu kila msafiri anaimani tofauti tofauti.


"Naomba Tuzingatie Kanuni taratibu na miongozo ilizowekwa na Mamlaka Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) mahubiri ndani ya mabasi hayaitajiki na endapo ikabainika basi linafanya huduma hiyohatua Kari za kisheria zitachukuliwa kwa dereva na Mmiliki wa gari hilo," Alisema Mkurugenzi huyo.


Aitoa ufafanuzi  juu ya baadhi ya magari kuwabagua baadhi ya abiria Johansen  Kahatano  Mkurugenzi wa Udhibiti Usafiri wa Barabarani Alibainisha tabia hiyo ni kosa kisheria na haivumiliki na endapo ikitokea mtu afanyiwa kitendo hicho apekeke malalamiko yake katika mamlaka husika.


" Tuliseme hili wazi Serikali ndio iliyokuwa na mamlaka ya Kutoa huduma ya usafirishaji lakini Serikali ikawapa jukuku hilo sekta binafsi ,"



"badala  ya Serikali Kutoa huduma wenyewe imewaachia sekta binafsi Kutoa huduma ya usafiri hivyo vitendo vya kubagua abiria vuachwe mara moja kwani abiria wote ni wananchi," Alisema Kahatano


Hata hivyo hatua hiyo imekuja ikiwa ni hivi karibuni Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Selemani Jafo kueleza madhara ya kelele na mitetemo isizo za lazima kwennye magari zinavyoathiri Afya ya binadamu ikiwemo afya ya akili na msongo wa Mawazo.


Pamoja na hayo amesema magari hayo ya abiria yanapokuwa na kelele husababisha abiria kukosa utulivu, kutokulala, kuongezeka kwa mapigo ya moyo na kupelekea shinikizo la damu, hivyo kanuni zimewekwa ili kulinda afya za binadamu na kuhimiza utunzaji wa mazingira kwa ujumla.


Aidha Mkurugenzi huyo alisema kuhusu kampeni ya LATRA kuyaingiza mabasi ya abiria kwenye mfumo wa tiketi mtandao ambapo hadi sasa tayari mabasi 550 kati ya 7000 yameshaingizwa kwenye mfumo huo.

No comments:

Post a Comment

Pages