HABARI MSETO (HEADER)


 


Breaking

July 27, 2022

Tamasha la Kimataifa la Dansi la Haba na Haba kufanyika Julai 29- 30 Dar, Wasanii wa Muziki watakiwa kutilia mkazo tamaduni za asili

 

Meneja Mradi wa ASSEDEVA, Upendo Manase.

Na Hussein Ndubikile,  Dar es Salam

Makumbusho ya Taifa na Nyumba ya Utamaduni kwa kushirikiana na Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Sanaa kwa Maendeleo ya Kijamii na Kiuchumi Katika Afrika (ASEDEVA)  wamewataka vijana wanaofanya sanaa ya muziki kuzingatia tamaduni za asili ili kuendelea kuutangaza urithi wa nchi.

Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Taasisi ya ASEDEVA, Isack Abeneko wakati akitambulisha Tamasha la Kimataifa la Dansi la Haba na Haba 2022 litakalofanyika Julai 29 hadi 30 mwaka huu jijini humo.

Amebainisha kuwa  lengo lao ni kuhakikisha wanawasaidia vijana kuweza kujikwamua kiuchumi kupitia sanaa zao wanazozifanya.

Abeneko amesisitiza kuwa taswira ya tamasha hilo ni kuwawezesha wasanii kupata mbinu mpya ambazo zinaweza zikawasaidia vijana hao kuboresha kazi zao za sanaa ili ziweze kuwa na ueledi.

‘Wiki hii kuanzia leo Tar 25 -30 tutakuwa na tamasha ambalo linaitwa Haba na Haba Internationa Dance Festival ambalo tumeanza na warsha na zipo za aina tano zikiwemo za ngoma za Asili kwa ajili ya kuwafundisha vijana wanaofanya miondoko ya kisasa kuzingatia tamaduni za asili asilia,kufaragua wasanii watakuwa wanafundishwa,masai dansi pia itakuwepo’amesema Abeneko

Ameongeza kuwa tamasha hilo litafanywa na wasanii tofauti tofauti akiwemo Fenando Anuang’a kutoka Ufaransa,Duduzile Voigts kutoka Ujerumani,Luanda Mori kutoka Swizland,Safi Theather kikundi cha asili cha nyumbani na Thami Mjela kutoka Afrika ya Kusini.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Achiles Bufure amesema dhamira Museam Arts Explosin –(MAE) ambalo linafanyika kila mwisho wa wezi ni kuwasaidia vijana wa kitanzania wanaofanya sanaa kutangaza kazi zao.

‘Sisi kama Makumbusho ya Taifa na Nyumba ya Utamaduni kama kawaida tumekuwa tukitoa nafasi kila mwisho wa mwezi kupitia program ya MAE ili wasanii wa kitanzania waweze kuonyesha kazi zao hivyo ASEDEVA wamepata nafasi hiyo kufanya kazi zao za kisanii’amesema Bufure

Nae, Meneja Mradi wa ASSEDEVA, Upendo Manase amefafanua kuwa  tamasha hilo ni la sita tangu kuanzishwa kwake ambapo wamekuwa wakihusisha sanaa ya ngoma za asili na masuala ya ubunifu.

Pia amesema tamasha hilo litaanza muda wa saa moja asubuhi na kwamba viingilio kwa wakubwa itakuwa Sh 10,000 na wanafunzi Sh 5,000 vyote vitalipwa kwa siku.

Tamasha hilo linatarajiwa kufanyika Julai 29 na 30 mwaka huu hivyo wananchi wametakiwa kutumia fursa hiyo katika kujitokeza kwa wingi ili kutangaza kazi ziweze kutambulika kitaifa na kimataifa.

No comments:

Post a Comment

Pages