HABARI MSETO (HEADER)


 


Breaking

July 26, 2022

TAMFI kutoa Mikopo kwa Taasisi za Fedha kusaidia Huduma ya Maji

 


Katibu  Mtendaji wa   TAMFI,  Winnie   Terry.

 

Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam


Wakati  Serikali   ikiwa  na  malengo  ya   kufikia  asilimia  95  ya  upatikanaji   wa  maji  nchini ifikapo  mwaka  2025,  Taasisi   ya   Tanzania Association  of  Microfinance   Institutions  ( TAMFI )  na   wanachama   wake  wamekuja  na  mpango  wa  kuunga mkono   juhudi za  Serikali  kwa  kutoa  mikopo   kwa  wadau  wa maji .

Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam na   Makamu   Mwenyekiti  wa TAMFI ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Yetu Microfinance,  Altemius  Millinga   katika   warsha   ya  Siku   moja ya kujadili masula ya maji    iliyowakutanisha    TAMFI  na  Taasisi  wanachama   wa   TAMFI  kutoka   Tanzania  Bara    na   Zanzibar  pamoja  Kampuni  ya  Water  org.

   Amebainisha kuwa  ili   kuunga  juhudi  za  Serikali  ya   awamu   ya  Sita  za   upatikanaji    wa  maji   wamejipanga   kufanikisha   upatikanaji  wa  huduma  hiyo  kwa kutoa  mikopo  kwa  ajili  ya   huduma  za  upatikanaji  wa  huduma    ya   maji  safi  na  maji  taka  kwenye  kila  kaya yenye   uhitaji.

Kwa  upande  wake  Katibu  Mtendaji wa   TAMFI,  Winnie   Terry   amefafanua kuwa   katika   kufanikisha   upatikanaji  wa  maji   wamejipanga  kutoa   elimu  na  kuratibu  warsha  na mafunzo   mbalimbali  na  kusaidia  taasisi  ndogo  za  kifedha   ili  waweze  kutoa  mikopo  inayohusiana  na  maji  na  maji  taka .

Takwimu  hapa  nchini   zinaonyesha   kuwa  upatikaji  wa  maji  vijijini   upo  kwa  asilimia  70  huku  mijini  ikiwa  ni  asilima  85.

Amesisitiza kuwa mpango huo ni wa miaka mitatu na kwamba TAMFI inalenga kuzisaidia taasisi za kifedha kwa kuzipa mikopo itakayokwenda kutatua changamoto za sekta ya maji nchini.

Nae Mwakilishi wa Taasisi isiyokuwa ya Kiserikali ya Water.org nchini, Upendo Massawe  amesema kuwa wanafanya kazi kwa ukaribu na TAMFI na kwamba walianza na programu ya kujua tafiti za maji na choo.  

No comments:

Post a Comment

Pages