Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, ametuma salamu za rambirambi kwa watu 10 wakiwemo wanafunzi 8 waliofariki katika ajali ya gari eneo la Mikindani mkoani Mtwara.
Rais Samia amesema "Nimesikitishwa na vifo vya wanafunzi 8 wa Shule ya Msingi King David na watu wazima wawili vilivyotokea leo eneo la Mjimwema, Mikindani, mkoani Mtwara. Natoa pole kwa wote waliopoteza jamaa zao. Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema na awajalie majeruhi wapone haraka."

Watu 10 wamefariki dunia katika ajali ya gari eneo la Mjimwema mkoani Mtwara. Taarifa za awali zinaeleza waliofariki ni wanafunzi nane, dereva na mama aliyekuwa ameomba lifti. Wanafunzi 19 wamejeruhiwa katika ajali hiyo inayohusishwa na kufeli kwa mafumo wa breki wa gari.
Watu 10 wakiwemo wanafunzi wanane wamekufa katika ajali ya gari asubuhi ya leo huko Mjimwema Manispaa ya Mtwara Mikindani Mkoani Mtwara, Mganga Mkuu wa Mkoa Dk. Hamad Nyembea amethibitisha.





No comments:
Post a Comment