HABARI MSETO (HEADER)


 


Breaking

July 25, 2022

Waziri Ndalichako azitaka Taasisi za Mafao kuacha Urasimu utoaji Mafao Wastaafu


Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi , Vijana Ajira na Watu Wenye Ulemavu Profesa Joyce Ndalichako amezitaka Taasisi zinazohusika na utoaji wa Mafao kwa Wastaafu kuacha Urasimu pindi wanapohitaji huduma ya kulipwa mafao yao.

Ameyasema hayo jijni Dar es Salaam katika Kongamano na Wazee Wastaafu Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) na PSSSF  na kwamba kumekuwepo na changamoto mbalimbali ikiwemo ya mapunjo ya mafao na kuwataka wakuu wa taasisi hizo kurekebisha kasoro hiyo.

"Mtu anapokuja hapa lazima aje na vielelezo vya mshahara na nyaraka nyingine za muhimu lakini kumekuwepo na urasimu usiokuwa wa lazima hivyo kusababisha usumbufu '" amesema Profesa Ndalichako.

Amebainisha kuwa kumekuwepo na baadhi ya Taasisi za Umma ambazo haziwasilishi michango ya wafanyakazi wao hivyo zitachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.

Ameongeza kuwa zipo pia baadhi ya taasisi binafsi ambazo haziwasilishi taarifa za mafao na kwamba zitabanwa kwa mujibu wa sheria.

Amewataka watendaji wa mifuko hiyo ya hifadhi ya jamii kuwaondolea ukuta wananchi wanapokwenda kutaka huduma ikiwemo ikiwemo kuonana na watendaji wakuu kwa ajili ya kuelezea malalamiko yao juu mafao yao kuwa madogo.

Pia, amesema kuwa vikao vya kujadili changamoto na kutatua changamoto za wastaafu vitakuwa endelevu ili kuhakikisha wanapata stahiki zao kwa wakati mwafaka.

Kwa upande wake,Chiku Said ambae ni miongoni mwa wastaafu waliofika katika kikao hicho cha kupeleka malalamiko kuhusu mafao amesema amefanya kazi na Wizara ya Afya tangu 1973 na kustaafu mwaka 2014 hadi kufikia leo Julai 22, mwaka 2022 hajapata mafao yake licha ya kufuatilia mara kadhaa.


No comments:

Post a Comment

Pages