HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 26, 2022

VEE MONEY: NATAKA PESA ZANGU


Msanii wa Bongofleva Vanessa Mdee maarufu kama 'Vee Money' ameibua leo baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu na kuamua kuwatolea uvivu kampuni ya kuuza na kusambaza muziki maarufu kama 'Mziiki' kwa kile alichodai kwamba anawadai pesa zake.

Vee Money amesema amejaribu kutumia njia nzuri ya kudai pesa hizo lakini imefikia hatua kampuni hiyo imepiga kimya, hata hivyo msanii huyo leo ametumia ukurasa wake wa Twitter kuandika malalamiko yake.

"Jamani pesa ya mziki zinatafutwa kwa shida kweli kweli na wasanii kuanzia kubuni hadi mpaka ifikapo kwa wananchi. Tafadhali @Mziiki nawaomba mnilipe pesa zangu kwa makubaliano tulionayo". alisema Vee Money

"Nimejaribu the professional way na team yangu sasa imefikia hatua ya nyie kutokujibu". alimalizia.


No comments:

Post a Comment

Pages