Na John Richard Marwa
Klabu ya Azam FC imethibitisha kuachana na aliyekuwa Kocha Mkuu wa kikosi chao, Mfaransa Denis Levagne baà da ya kuwa na muendelezo mbaya katika michezo ya hivi karibuni.
Ni kama kumla kichwa Levagne Usiku wa Giza, unaweza kueleza hivyo ni mara baà da ya taarifa za kuachana na kocha huyo kutolewa usiku mzito kweye mitandao ya kijamii ya Klabu hiyo.
Azam wamefikia hatua hiyo ikiwa ni siku moja baà da ya kupoteza mchezo wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara dhidi ya KMC FC hapo jana Kwa mabao (2-1) katika Dimba la Uhuru.
Hata hivyo Azam FC siku kadhaa zilizopita imetoka kutolewa katika michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika CAF CC na Al Akhdar ya Libya.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa usiku huu imeeleza kuwa uamuzi huo umefikiwa kutokaana na maslahi mapana ya kiufundi ndani ya Klabu.
"Bodi ya Azam FC imesitisha mkataba na Denis Lavagne, kama kocha mkuu, kuanzia leo, Oktoba 22, 2022.
"Uamuzi huo ni kwa maslahi mapana ya klabu na mustakabali wa mradi wake wa maendeleo ya kiufundi." Imeeleza taarifa hiyo na kuongeza kuwa
"Denis Jean Lavagne, raia wa Ufaransa, alijiunga na Azam FC Septemba 7 mwaka huu akisaini mkataba wa mwaka mmoja uliomtaka aifikishe klabu kwenye angalau hatua ya makundi ya mashindano ya Afrika."
"Kwa bahati mbaya mahitaji hayo ya kimkataba hayakufikiwa hivyo bodi ikafikia uamuzi huu."
Kwa sasa timu itakuwa chini Kalimangonga Sam Daniel Ongala na Agrey Moris hadi hapo itakapotangazwa vinginevyo."
Hata hivyo taarifa hiyo imetoa shukrani kwa Kocha huyo kwa muda ambao amekuwa na timu.
"Bodi inamshukuru Lavagne kwa jitihada zake za kuisaidia klabu yetu na weledi mkubwa aliouonesha alipokuwa nasi. Aidha inamtakia kila la heri huko aendako."



No comments:
Post a Comment