HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 22, 2022

TYSON FURY KUREJEA ULINGONI DESEMBA


 

Na Mwandishi Wetu

BONDIA muingereza, TYSON FURY, atarejea ulingoni Desemba 03 mwaka huu, kupambana na DEREK CHISORA, katika pambano lao la tatu, litakalopigwa uwanja wa Tottenham Hotspur, jijini London.

FURY, 34, atautetea ubingwa wake wa WBC uzito wa juu, kwa mara ya tatu dhidi ya bondia huyo, aliyemchapa mara mbili, hapo kabla.

Waingereza hao, walizichapa mara mbili mwaka 2014 na 2011, ambapo FURY alishinda kirahisi mapambano yote mawili.

FURY, alikuwa kwenye mazungumzo ya kupambana na ANTHONY JOSHUA, mwezi Desemba, lakini makubaliano hayo yalivunjika baina ya kambi zote mbili.

Bingwa huyo wa dunia, hajapigwa kwenye mapambano 32, wakati CHISORA, 38, anayekaribia mwisho wa karia yake ya masumbwi amepoteza mapambano matatu kati ya manne ya mwisho.

Pia siku hiyo bondia kutoka Afrika kusini, KEVIN LERENA atapambana na muingereza DANIEL DUBOIS, ambaye atakuwa akilitetea taji lake la WBA 'Regular' uzito wa juu.

No comments:

Post a Comment

Pages