HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 22, 2022

NABI TUTACHEZA DARBY KIBINGWA NA HESHIMA

 


Na Mwandishi Wetu

Kocha Mkuu wa klabu ya Yanga Nasreddine Nabi
Kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Simba SC, amesema wanaingia kwenye Mchezo huo kucheza kikubwa kwa kiwaheshimu wapinzani wao.

Nabi akizungumza na vyombo vya Habari amesema wanaingia kwenye mtanange huo wakiwa na kumbukumbu ya kutolewa Ligi ya Mabingwa hivyo wanakila sababu ya kuibuka na ushindi hapo kesho.


“Mechi ya derby ni mechi kubwa ambayo imekuja baada ya mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika, kila mchezaji atajituma lakini akikumbuka kumheshimu mpinzani.”

"Desturi ya Yanga ni kuuchezea mpira na kupiga pasi, mimi sio kocha ninaecheza na mabeki 10.
Hata tulivyocheza Sudan mashabiki wa Sudan walifurahi wakasema Yanga inacheza mpira mzuri na hata media za Sudan ziliisifia Yanga kwa kucheza mpira mzuri.” ameongeza kuwam

"Tutakwenda kuwapa furaha mashabiki na mpira wetu uleule mashabiki watafurahi. Niwashukuru mashabiki wa Yanga kwa kiasi kikubwa walikuwa upande wangu ninawaahidi kuwapa furaha.”

"Football ni pale refa anapopuliza filimbi ndio inapoanza na football inapoisha ni refa anapopuliza filimbi hauwez kukumbuka sijui Simba amefuzu makundi au Yanga hajafuzu football haiko hivyo.”
 Kocha Nabi

No comments:

Post a Comment

Pages