HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 23, 2022

TANZANIA YASHINDWA KUTAMBA KWA NIGERIA


 

Na Mwandishi Wetu

Timu ya Taifa ya Tanzania chini ya miaka 23 imeshindwa kutamba mbele ya vijana wenzao wa Nigeria mchezo wa mkondo wa kwanza kuwania kufuzu Fainali za Afcon U23.

Tañzania U23 iliingia Dimbani hapo kumenyana na Nigeria Dimba la Benjamin Mkapa mtanange ulitamatika kwa sare ya bao (1-1).

Ulikuwa mchezo mzuri na bora kwa timu zote mbili huku zikigawna vipindi. Nigeria walitakata kipindi Cha kwanza na kufanikiwa kujipatia bao la Uongozi kwa mkwaju wa penati.

Tañzania U23 ilirejea mchezo kipindi cha pili mara baada ya mwalimu Hemmed Morocco kufanya mabadiliko kadhaa.

Kuingia kwa Tepsi Evans kuliongeza kasi ya mashambulizi kwenye safu ya mwisho ya Nigeria na kufanikiwa kupata mwaju wa penati uliowekwa kimiani na Ally Msengi.

Mara baada ya mchezo huo Kocha Hemed Morocco alisema vijana walicheza vizuri na anaamini wataenda kushinda.

"Ilikuwa mechi ngumu lakini wachezaji wajitahidi kwa sababu tulikuwa tunacheza na timu kubwa, kipindi cha kwanza tuliwaheshimu kiasi cha wao kuutawala mchezo.

"Dakika 90 za kwanza zimemalizika na Kwa jinsi tulivyocheza hapa niwahidi Watanzania tunaenda kupata matokeo huko kwao na kusonga mbele" amesema Morocco.

Tañzania U23 itasafiri wiki ijayo kuelekea Nigeria kwa ajili ya mchezo wa marejeano utakaopigwa mwishoni mwa juma lijalo.

No comments:

Post a Comment

Pages