HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 21, 2023

Kiongozi wa Mwenge aipongeza Same

Na Mwandishi Wetu

WILAYA ya Same mkoani Kilimanjaro imepongezwa kwa kusimamia fedha na miradi ya  maendeleo inayotelezwa wilayani hapo.

Pongezi hizo zimetolewa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka 2023, Abdallah Kaimu wakati akikagua miradi saba yenye thamani ya shilingi bilioni 3.6 iliyotekelezwa.

Kaimu amepongeza uongozi wa wilaya hiyo wakiongozwa na mkuu wa Wilaya Kasilda Mgeni kwa usimamizi mzuri wa miradi inayotekelezwa katika eneo hilo ambayo ni ya maji, afya, elimu, barabara na mingine.

Kiongozi huyo amesema katika miradi yote saba iliyopitiwa na Mwenge wa Uhuru imeonekana kutekelezwa katika ubora.

"Tumefanya ukaguzi wa kina kujiridhisha na ubora na viwango vinavyo hitajika, ukaguzi wa nyaraka na viambatanishi muhimu, miongozo mbalimbali katika utekelezaji wa miradi ya serikali na kujiridhisha hakuna dosari yoyote," amesema.

Amesema mafanikio hayo yanatokana  na usimamizi mzuri wa viongozi waliopewa jukumu la kumsaidia Rais Samia Suluhu Hassan  na serikali yake katika kuboresha huduma.

Miongoni mwa miradi hiyo iliyopitiwa ni ukarabati wa kiwango cha zege mita 810 za eneo korofi katika Barabara ya Hedaru-Vunta-Myamba, mradi unaotekelezwa na Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA) Wilaya ya Same.

Awali akitoa taarifa ya Ujenzi wa Maeneo hayo korofi Meneja wa TARURA Wilaya ya Same, Mhandisi James Mnene alisema ujenzi wa maeneo korofi ya Barabara ya Hedaru-Vunta-Myamba yenye urefu wa Mita 810 umegharimu takribani shilingi Milioni 655.5 na utamilika mwaka huu.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Same Kasilda Mgeni, Mkuu wa wilaya Hai Amir Mkanipa alisema ukarabati unaofanyika  pamoja na kuboresha huduma utaongezeko mapato ya halmashauri kwa wafanyabiashara kupata urahisi wa kusafirisha mizigo.

Mbunge wa Jimbo la Same Mashariki Anna Kilango amemshukuru Serikali ya Rais Samia kwa kuwakomboa wananchi wa Vuntaa na Mamba Miamba kwa kuleta fedha nyingi kukamilisha miradi mikubwa ya maendeleo.

No comments:

Post a Comment

Pages