Na Victor Masangu, Pwani
Jumla
ya wachezaji wapatao 120 wamechaguliwa kwa ajili ya kuunda kikosi cha
timu ya Mkoa wa Pwani kitakachoshiriki katika mashindano ya Umoja wa
michezo na sanaa kwa shule za sekondari Tanzania (UMISSETA) ngazi ya
Taifa itakayoanza kutimua vumbi Juni 15 hadi 25 mwaka huu mkoani
Tabora.
Akizungumza na
waandishi wa habari Afisa michezo wa Mkoa wa Pwani Grace Buleta amesema
kwamba wachezaji hao wamechaguliwa kutokana na uwezo na vipaji
walivyonavyo katika fani ya michezo mbali mbali.
Buleta
alitasema hayo wakati wa halfa ya kutangzwa kwa kikosi cha wachezaji
iliyofanyika katika viwanja vya shirikika la elimu Kibaha na kuhudhuliwa
na viongozi mbali mbali wa serikali wakiwemo walimu,Wanafunzi pamoja na
wadau wa michezo.
Afisa
michezo huyo alisema kwamba wachezaji hao wataingia kambini kwa kipindi
cha muda wa siku tano kwa ajili ya kujiandaa na kujinoa vilivyo kabla ya
kuanza safari ya kuelekea katika mashindano ya Kitaifa mkoani Tabora
tarehe 14 mwezi huu.
"Tunashukuru
tulikuwa na wachezaji wapatao 700 hapo awali lakini baada ya kufanya
mchujo tumefanikiwa kupata wachezaji wapatao 120 ambao ndio
watakaouwakilisha Mkoa wa Pwani katika mashindano ya Taifa mkoani
Tabora,"alisema Buleta.
Kadhalika
aliongeza kuwa katika mashindano ya mwaka huu wachezaji wamejipanga
vilivyo kuweza kuibuka na ubingwa wa Kitaifa kutoka na kujiandaa
vizuri katika michezo mbali mbali watakayoshiriki.
Amebainisha
michezo ambayo watashiriki katika michuano hiyo ni pamoja na
Netiboli,mpira wa miguu,kikapu,wavu,mpira wa mikono,riadha,fani za
ndani,ngoma,kwaya sambamba na mziki wa kizazi kipya.
Katika
hatua nyingine alimshukuru kwa dhati mdau wa michezo ambaye pia ni
Mjumbe wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi (CCM) Mussa Mansoor kwa
kuchangia vifaa mbali mbali vya michezo kwa timu ya Mkoa ili iweze
kufanya vizuri.
Kwa
upande wake Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM Mussa Mansoor alisema lengo
lake kubwa ni kusaidia kukuza sekta ya michezo kuanzia ngazi za chini
kwani michezo kwa sasa ni fursa za ajira.
Pia
aliongeza kuwa ametoa vifaa mbali mbali vya michezo kwa lengo la
kuwasaidia vijana waweze kupata fursa ya kuonyesha na kuibua vipaji vyao
walivyonavyo.
Naye
Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani ambaye alikuwa mgeni rasmi katika halfa
hiyo amewataka wanamichezo ambao wamechaguliwa kuhakikisha wanakuwa na
nidhamu ili waweze kufanya vizuri katika michuano hiyo ngazi ya Taifa.
No comments:
Post a Comment