Na Mwandishi Wetu
BENKI ya NMB imeingia mkataba wa mashirikiano na Klabu ya Yanga kwa ajili ya kuwawezesha wananchama na mashabiki kupata kadi kupitia matawi yao yote nchi nzima.
Zoezi hilo limefanyika asubui ya leo Makau Makuu ya Benki hiyo jijini Dar es Salaam ambapo viongozi wa pande zote wamesaini makubaliano hayo.
"Kwa kutambua umuhimu wa sekta ya michezo nchini, leo tumeingia makubaliano na timu ya Yanga na kuwa Benki ya kwanza nchini kuwawezesha mashabiki na wanachama wa Yanga kupata kadi za uanachama kupitia matawi yote ya NMB yaliyoenea nchi nzima.
Taarifa imeeleza kuwa baada ya kusaini makubaliano hayo, ushirikiano utalenga maeneo yafuatayo:
"Kutumia mtandao mpana unaojumuisha matawi zaidi ya 228 kote nchini kufanya usajili wa wanachama na mashabiki wa Yanga, wakiwemo wenye umri chini ya miaka 18. Kadi hizi maalum zitakua nembo za Yanga na NMB.
"Mwanachama wa Yanga atalipia Shilingi 34,000 kama kianzio cha kupata kadi ya Yanga (Shilingi 5,000 ni malipo ya kadi, 5,000 amana ya kuanzia na shilingi 24,000 ni ada ya Mwanachama kwa mwaka mzima).
"Kadi za mashabiki ambao sio wanachama - Malipo yatakua shilingi 22,000 tu (shilingi 5,000 ni ya kadi, 5,000 amana ya kuanzia na shilingi 12,000 ni ada ya shabiki kwa mwaka mzima).
"Kadi hizi hazitakua za uanachama/ushabiki tu, pia zina uwezo wa kufanya kazi kama kadi ya Benki! Unaweza kufanya miamala yote ya kibenki ikiwemo kuiwekea pesa, kutoa hela katika ATM na kufanya malipo mtandaoni na katika vituo vya malipo (POS).
"Wanachama wanaweza kupata kadi za Malipo ya Kabla (Prepaid Card) ambayo huitaji kuwa na akaunti nasi na kufanya malipo kwa kupitia mtandao au kwenye Point of Sales (POS).
"Wanachama na mashabiki watanufaika na huduma na ofa mbalimbali za NMB ikiwemo mikopo isiyokua na dhamana (Mshiko Fasta) na punguzo la bei wakifanya malipo kupitia NMB Lipa Mkononi (QR).
"Tutawezesha matawi ya Yanga zaidi ya 900 nchi nzima kutoa huduma za uwakala wa NMB
"Mbali na huduma za uanachama, tutakua na Bima ya Mwananchi ambayo itakua na gharama nafuu." Imeeleza.
Usajili huo utaanza rasmi Julai 10, 2023 kwenye matawi yote ya NMB. Wananchi wanatakiwa kutembelea tawi lililo karibu yao kupata maelekezo zaidi.
No comments:
Post a Comment