Na Mwandishi Wetu, Arusha
Wakati Shule ya Sekondari Sombetini wakilia na uhaba wa madawati 363, Benki ya
NMB imefanikiwa kuwakabidhi msaada wa viti na meza 100 vyenye thamani
ya shilingi million 10.
Msaada huo umetajwa kuwasaidia wanafunzi 100 pa kukalia, huku wakiomba wadau wengine kujitokeza.
"Tunashukuru
sana kutupunguzia pengo hili kubwa, hakika mmetusogeza sana, kwani
tulikuwa na uhitaji wa viti 363 na sasa mmetupa 100 na kufanya idadi ya
viti shuleni hapa kufikia 1362 ukiachana na zile 1262 zilizokuwa
zinategemewa na wanafunzi wote 1625, msituchoke tukija kuomba vingine
263 zilizobaki" alisema mwalim mkuu wa shule ya Sombetini Bertha John
Akizungumza
wakati wa makabidhiano, meneja kanda ya kaskazini wa Benki ya NMB,
Baraka Ladislaus alisema msaada huo ni muendelezo wa utaratibu wao wa
kurudisha faida kwa kuhudumia jamii wanaozidi kuiwezesha Benki hiyo
kufanya vizuri nchini.
"Benki
ya NMB mwaka huu tumetenga zaidi ya billion 6.2 kwa ajili ya kuhudumia
jamii ambapo ukiachana na mazingira na Afya, pia Elim ni moja ya
kipaumbele chetu muhimu kutokana na kutambua ukweli kuwa ndio msingi
sana kwa maendeleo ya Taifa lolote hapa duniani" alisema Baraka
Aliongeza
kuwa msaada huo wa viti na madawati 100 vyenye thamani ya shilingi
million 10, sio mwanzo na hautakuwa mwisho wa kusaidia serikali katika
kutatua changamoto zinazoikabili sekta ya Elim, Afya na mazingira
lakini pia majanga mbali mbali yanayojitokeza nchini.
"Tunatambua
juhudi kubwa za serikali chini ya Rais wetu Samia Suluhu za kusimamia
upatikanaji wa huduma bora kwa wananchi, hivyo sisi kama wadau tunao
wajibu wa kuunga mkono, kusaidia na kuwa mstari wa mbele katika kuchagia
utatuzi wa changamoto zinazojitokeza katika jamii" alisema meneja huyo
wa NMB.
Alisema kuwa
moja ya mafanikio makubwa waliyoyapata ni kufungua matawi 229 na
kusambaza mashine za kutokea huduma zaidi ya 800 huku wakiwa na zaidi
ya mawakala 20, 000 nchi nzima
"Kwa
sasa NMB tumefika mikoa na Wilaya zote nchini huku tukizindua kampeni
mbali mbali za kutoa masuluhisho ya huduma za kifedha na mikopo kwa
wateja wetu ikiwemo ',onja unogewe ' , 'hati fungani' na zinginezo
nyingi"
Akipokea msaada
huo mkuu wa Wilaya ya Arusha Felician Mtahengerwa aliipongeza Benki ya
NMB kwa kuwa msaada mkubwa kwa jamii na serikali kupitia misaada yao
katika sekta ya Afya na Elim huku wakiwataka kutanuka zaidi kimataifa.
"Hakika
nawapongeza sana kwa kuwa Benki namba moja nchini kutambua na kutatua
changamoto zinazoikabili jamii zilizokuwa ziigharimu serikali, hivyo
nawapa changamoto kubwa sasa mtanue matawi yenu nje ya nchi ili
kuwahudumia na watanzania walioko nje lakini watalii wanaoingia nchini
kutoka nje"
Zaidi
aliwataka kuunga mkono pia juhudi za halmashauri za kuweka Jiji safi kwa
kutoa msaada wa ndoo za kukusanyia taka (dustbin) Ili zisambazwe mjini
katika kuweka Arusha katika hali ya usafi na kuvutia watalii zaidi.
Akitoka
shukrani kwa msaada huo, mmoja wa wanafunzi Joan Mremi alisema samani
hizo zimekuja wakati muafaka wakielekea kufanya mitihani yao ya kidato
cha nne ambapo wangelazimika kuwanyang'anya wanafunzi wenzao wa madarasa
ya chini viti Ili kufanya mitihani kwa uwiano wa mwanafunzi mmoja kiti
kimoja.
"Tunasema Asante
sana kwa Benki ya NMB kuonyesha ukaribu wao kwetu kivitendo, na
tunaahidi kutumia viti hivyo kuongeza ufaulu kwani wanafunzi wengi sasa
watakuwa na viti vya kukalia sio kubebana wala kukaa kwa zamu"
No comments:
Post a Comment