HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 16, 2025

Dakika 90 za mtego Ngao ya Jamii Simba, Yanga

Leo ndio leo katika Dimba la Benjamin Mkapa ambapo miamba ya Soka la Tanzania Simba SC na Yanga SC kuulizana maswali magumu ndani ya dakika 90 za mchezo wa ufunguzi wa msimu wa mashindano 2025/26 maarufu kama Ngao ya Jamii.

Kila timu inaingia na swali la kujijibu kabla ya kuwaburudisha wahafidhina wa Soka, Simba licha ya kuwa timu namba tano kwa ubora Barani Afrika hawapata matokeo katika michezo mitano mtawalia mbele za watani zao.

Wakati Yanga wakiwa na swali gumu zaidi la kuendeleza ubabe kwa mtani wske katika mchezo wa sita mtawalia. Ikumbukwe kuwa miamba hiyo juma lililopita zilicheza michezo yao ya kilele cha Simba Day na Mwananchi Day huku zikiibuka na ushindi licha ya kutoonyesha kiwango bora katika mchezo hiyo.

Mtanange huo utapigwa majira ya saa 11 kwa saa za Afrika Mashariki katika Dimba la Benjamin Mkapa huku pilato akiwa ni Ahmed Arajiga.

Nani kucheka leo na kuuanza msimu kwa mguu wa kulia? ni dakika 90 pekee zinajua majibu ya swali hlo.


 

No comments:

Post a Comment

Pages