Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), imetoa gari aina ya Toyota Hilux, Double Cabin yenye thamani ya takribani TSh.Milioni 100.7 kwa Shule ya sekondari Kiwani iliyopo mkoani, Pemba, Zanzibar.

Akizungumza na wanahabari shuleni hapo, Mkuu wa shule hiyo, Ally Sima Makame alisema gari hilo ni kwa ajili ya shughuli za utawala na kuwahudumia watoto inapotokea mmojawapo akapatwa na changamoto yoyote na kuhitaji kukimbizwa hospitali ya Mkoani ambayo haipo jirani na shule.
Makame alisema kuwa gari hiyo imekuwa msaada mkubwa kwao na imeonyesha jinsi gani Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi anavyojali watu wake na kuwa tayari kutoa msaada kila unapohitajika.
“Hivi sasa shughuli nyingi za utawala zimefunguka na tunaweza kufanya mambo mengi kwa haraka tofauti na mwanzo” alisema na kuongeza kuwa upande mwingine ujenzi wa shule za ghorofa umesaidia kupunguza utoro kwa wanafunzi.
Alisema kuwa hivi sasa hakuna utoro shuleni na kwa kuwa mazingira ya kusomea, kujifunza na kufundishia yameboreshwa hivyo hata ufaulu umeongozeka shule za msingi na anabainisha kuwa awali ilikuwa na watoto 234 lakini hadi hivi sasa idadi imepanda na kufikia wanafunzi 909.
Alisema mkuu huyo wa shule kuwa awali ilikuwa ya mabanda hivyo kuchangia utoro na watoto kukosa ari ya kujjisomea huku ikikabiliwa na uhaba wa walimu ambao sasa wamefikia 26 kutoka 13 na ni ya ghorofa nne ikiwa na madarasa 45, maabara za sayaysi 3 na maktaba ya kisasa inayosimamia na Idara ya Maktaba ya Taifa.



No comments:
Post a Comment