WEKUNDU wa Msimbazi Simba SC, imefuzu raundi ya pili Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF CL 2025/26), licha kubanwa mbavu na Gaborone United ya Botswana na kumaliza dakika 90 kwa sare ya bao 1-1 kwenye dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
Simba iliyoongozwa na kocha wa muda Hemed Suleiman 'Morocco', imefanikiwa kuingia hatua ya 32, ambako sasa itapepetana na Nsingizini Hotspurs ya Eswatini, ambayo imeiondoa Simba Bhora ya Zimbabwe kwa mikwaju ya penalti 4-1, baada ya kila moja kushinda mechi ya nyumbani kwa bao 1-0.

Wekundu wa Msimbazi watalazimika kubadilika ikiwa inahitaji kuwatupa nje Hotspurs na kufuzu hatua ya makundi, kwani kiwango ilichokionesha leo nyumbani kilikuwa kibovu na nusura watupwe nje, kama sio umahiri na ubora wa mlinda mlango Moussa Camara, ambaye aliumia na kutolewa na nafasi yake kujazwa na Yakoub Suleiman.
Jean Charles Ahoua aliifungia Simba mkwaju wa penalti uliotokana na madhambi aliyofanyiwa Morice Abraham katika dakika za nyongeza za kipindi cha kwanza, lakini nafasi mbili za wazi alizoshindwa kutikisa nyavu za Gaborone United, zimemuingiza kwenye lawama kutoka kwa mashabiki.
Gaborone United walisawazisha bao hilo kunako dakika ya 66 kupitia kwa Lebogang Ditsele, na tangu hapo Simba ikajiingiza kwenye presha kubwa, kwani walikaribia kusukumwa nje ya mashindano hayo ya pili kwa ukubwa ngazi ya klabu barani Afrika.
September 28, 2025
Home
Unlabelled
Simba yavuka kinyoonge CAF CL, sasa kuwavaa 'Watoto wa Mfalme Mswati'
Simba yavuka kinyoonge CAF CL, sasa kuwavaa 'Watoto wa Mfalme Mswati'
Share This
About HABARI MSETO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.






No comments:
Post a Comment