NA DENIS MLOWE, IRINGA
MRATIBU
wa kampeni jimbo la Iringa Mjini Salvatory Ngelela amesema kuna kila
sababu za wanachi wa Kata ya Kitwiru kukipigia kura za kishindo Chama
cha Mapinduzi karika uchaguzi wa Oktoba 29 mwaka huu kwa Rais , wabunge
na madiwani kutokana na mambo mengi waliyofanya kutokana na ilani
iliyopita.
Akizungumza kwenye mkutano wa
kampeni wa chama hicho uliofanyika katika kata ya Kitwiru, Ngelela
alisema kuwa ilani ya CCM iliyopita na waliyofanya kwa wananchi
imetekelezwa kwa asilimia kubwa hivyo wanaomba ridhaa tena kwa wananchi
kwa miaka 5 inayokuja ili kuendeleza pale walipoishia.
Ngelela
ambaye pia ni Mjumbe wa kamati ya siasa ya wilaya alisema kuwa
yaliyoyafanywa miaka 5 iliyopita na miaka 5 inayokuja ni mazuri zaidi na
ndio maana kuna baadhi wamekimbia uchaguzi kwa kuhofia wananchi
watapotezea katika kuwapa kura.
Alisema kuwa
CCM wanamgombea urais ambaye amefanya makubwa kitaifa kwa muda mfupi na
yanaonekana kwani ilani aimeitekeleza kwa asilimia zote hivyo wananchi
wajitokeze kwa uwingi kumpa kura mama Samia.
Akizungumzia
mgombea Ubunge wa Jimbo la Iringa mjini, alisema kuwa CCM wamewapa
mgombea ambaye amejitosheleza kwa kila kitu kuanzia elimu hadi
ushirikiano kwa wananchi hivyo wana kila sababu ya kujivunia na kumpa
kura za kishindo Fadhili Ngajilo.
Ngelela
alisema kuwa Ngajilo sio mtu wa danadana ni mtu wa vitendo sio mtu wa
porojo kama ambavyo baadhi ya wagombea wa vyama vingine wanaleta porojo
kwenye maisha ya wananchi.
Alisema kuwa
Unapokuwa kiongozi unatakiwa kuwa mfariji wa watu wa Iringa hivyo katika
hili Ngajilo ni mtu sahihi kwa wana Iringa na mtu sahihi kutupeleka
kwenye nchi ya ahadi.
Alisisitiza kuwa
usithubutu kususa chakula kwa mtu mwenye njaa kali hivyo CCM wana njaa
kali ya kuleta maendeleo ya nchi na kama chama tunashindana na yoyote
anayekuja mbele yetu na tunafanya kampeni ili kuomba ridhaa kwa wananchi
kutokana na njaa ya maendeleo.
"Huwezi kushika nchi bila
kuomba ridhaa kwa wananchi tarehe 29 wananchi watafanyaka kazi moja ya
kuchaigua ccm kuongoza nchi",Alisema
Naye
Mwenyekiti wa CCM wilaya iringa Said Rubeya alisema kuwa ahadi
ziliahidiwa katika kata ya Kitwiru zimefanyika zote na kutolea mfano
shule ya msingi Uyole, sekondari Kwavava ambazo waliahidi kujenga
wamefanya hivyo.
Aliongeza kuwa ahadi ya kituo
cha afya Kitwiru imetekelezwa na wananchi hivi karibuni wataanza kupata
huduma hivyo kama chama wamekuja tena kuahidi ya miaka 5 ambayo
watawafanyia wananchi.
Alisema kuwa kama chama wameleta ilani kwenu kwa ajili ya maendeleo ya miaka mitano ambayo imemgusa zaidi mwananchi.
"Naombeni
kura nyingi kwa mama na ukiangalia mama kama ameshinda ila tunahitaji
kura nyingi sana kwa ajili ya mama kwani aliyofanya kwa nchi ni makubwa"
Alisema
Kwa upande wake mgombea udiwani wa
kata hiyo, Rahim Kapufi Ameomba kura kuwa diwani ili aweze kusukumia
ajenda maendeleo katika kata hiyo kwenye baraza madiwani.
Alisema
kuwa wananchi wampe kura Mgombea urais Dk. Samia Suluhu Hassan mgombea
ubunge wa Jimbo la Iringa Mjini ,Fadhil Ngajilo na udiwani katika
uchaguzi mkuu wa Oktoba 29 mwaka huu
Alisema
kuwa akichaguliwa kuwa diwani atahakikisha changamoto mbalimbali katika
kata hiyo zinashughulikiwa ikiwemo ya ukamirishaji kituo cha afya.
Alisema
kuwa akiwa diwani atahakikisha Kuwezesha uchumi kwa kina mama na vijana
bila kusahau wazee kwani suala la mikopo zimeongezeka kutoka bilioni 2
hadi 9 hivyo wananchi watapata mikopo isiyoumiza.
Aliongeza
kuwa atahakikisha Suala maeneo ya kurasimisha makazi tutafanya kata
zima, kupima viwanja ambavyo havijapimwa ili wananchi wamiliki maeneo
halali.
Kapufi aliongeza kuwa atahakikisja Barabara za mitaa zitakwenda kurekebishwa ndio itakuwa kazi ya kwanza ili ziweze kupitika.
Mgombea
ubunge Iringa mjini kwa tiketi ya CCM, Fadhili Ngajilo alisema kuwa
kwa upande wake amejiandaa kuwatumikia wanachi kwa ukaribu zaidi na
kuondoka ile tabia ya kiongozi kuwa mbali na wananchi.
Alisema
kuwa atakuwa karibu na wananchi hivyo atawafikia wananchi kwa wakati na
kuhakikisha kata zima Kitwiru ibadilike ifanane na manispaa.
Alisema
kuwa atahakikisha kituo cha afya kianze kazi mara baada ya kuwa mbunge
na ataendelea kunisikia katika mambo mbalimbali ya kimaendeleo katika
jimbo la Iringa mjini.
Alisema kuwa
atahakikisha Daraja la Kitwiru linalounganisha kata jirani ya Isakalilo
lianze kujengwa kwa uharaka ili kuileta karibu kata hiyo na utalii
kwani itakuwa njia rahisi kupitika.
Aidha
alisema kuwa katika kata ya Kitwiru kuna kero ya soko lao la mazao
hivyo nitapambana kuweza kujengwa kwa soko hilo na atalibeba kwa ajili
ya wananchi.
Upande wa maji Ngajilo
alisema kuwa kuna sehemu hayajafika hivyo ni kazi ambayo
atashughulikia kwa haraka kwa kuwaona Iruwasa pindi atakapochaguliwa.
Aidha
alisema kuwa suala la mikopo kwa kina mama, vijana kujishughulisha na
shughuli mbalimbali kuhakikisha na mafanikio yao na wazee msiwe na
wasiwasi na watoto pia.
Ngajilo aliomba
Wananchi kumpa ushiirikiano akiwa mbunge ili waharakishe maendeleo ya
jimbo la Iringa na kuwaomba kura za kishindo kwa mgombea urais Dk Samia
Suluhu Hassan, na madiwani wa kata zote kupitia Chama Cha Mapinduzi.




No comments:
Post a Comment