HABARI MSETO (HEADER)


 


Breaking

April 21, 2026

CRDB Yazindua Msimu wa Pili wa Graduate Trainees, Maelfu Waomba — 26 Wateuliwa

CRDB Bank imezindua rasmi msimu wa pili wa programu ya Graduate Trainees, hatua inayoonyesha dhamira ya benki hiyo kuendelea kukuza vipaji vya vijana na kuandaa kizazi kipya cha viongozi wa sekta ya fedha.


Akizungumza wakati wa uzinduzi, Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Abdulmajid Mussa Nsekela, alisema benki inaendelea kuwekeza kwa vijana wenye ubunifu na maono mapana ili kuimarisha uongozi wa kesho.



Maombi Zaidi ya 4,800, Waliochaguliwa Ni 26 Tu

Kwa mujibu wa Nsekela, programu hiyo ya miaka mitatu ilipokea maombi zaidi ya 4,800 mwaka huu, lakini ni vijana 26 pekee ndio waliofaulu baada ya mchujo mkali.


Tanzania imetoa washiriki 18

Burundi imetoa washiriki 4

Democratic Republic of the Congo (DRC) imetoa washiriki 4

Programu hii pia inajumuisha vijana kutoka maeneo ambayo benki hiyo inaendesha shughuli zake, ikiwamo Dubai.


Mafanikio ya Msimu wa Kwanza Yamefungua Milango Mpya

Mkurugenzi wa Utumishi, Godfrey Rutasingwa, alisema mafanikio ya msimu wa kwanza—uliowahusisha washiriki 30—ndio msingi wa kupanua programu hiyo mwaka huu.



Ameeleza kuwa washiriki wa awali walitoa mchango mkubwa katika ubunifu wa teknolojia na mifumo ya kidijitali ndani ya benki.



Washiriki Wapya Wazungumza

Mmoja wa washiriki wa mwaka huu, Frank Mukwabe, amesema programu hiyo imekuwa mkombozi kwa wahitimu wapya ambao hukosa uzoefu wanapoingia kwenye soko la ajira.

“Hii ni nafasi muhimu kwetu kujifunza kwa vitendo, kukuza taaluma na kuwa viongozi wa siku zijazo katika sekta ya fedha,” alisema.

Programu imeanza rasmi na inatarajiwa kuwajengea washiriki uwezo katika maeneo ya uongozi, teknolojia ya fedha (FinTech), usimamizi wa biashara, pamoja na ubunifu wa bidhaa za benki.




No comments:

Post a Comment

Pages